TATIZO LA MIKOPO KUPATIWA UFUMBUZI
Wananchi
mbalimbali wakiingia katika Maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa
yanayofanyika katika viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa kwa
ajili ya kujipatia bidhaa mbalimbali.Maonyesho hayo yameanza jana hii
Jijini Dar es salaam.Picha n Daudi Manongi,MAELEZO
Askari wa
JKT pamoja na FFU wakihakikisha usalama wakati wananchi wakiingia
katika viwanja vya Mwalimu Nyerere kuangalia bidhaa mbalimbali baada ya
maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa kuanza jana jijini Dar es
salaam.
Afisa
Habari Idara ya Habari,MAELEZO Bi.Immaculate Makilika akizungumza jambo
na Afisa Biashara kutoka Wizara ya Viwanda ,Biashara na Uwekezaji
Bw.Baruti Mwaigaga(kushoto) katika banda la Wizara hiyo viwanja vya
Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Mwananchi
akiangalia moja ya bidhaa zinazotengenezwa na kikundi cha African
Flowerless fashioncha Arusha kinachouza bidhaa zake nje ya nchi.Kulia ni
Afisa wa kikundi hicho Bi.Suzana Mwalongo.
Mafundi
wakiendelea na upakaji rangi katika banda la CRDB katika Maonyesho ya 40
ya Biashara ya Kimataifa viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar e
Salaam.
Na: Immaculate Makilika- MAELEZO, Dar es salaam.
SERIKALI
kupitia Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji imeandaa mkakati ya
kulipatia ufumbuzi tatizo la ukosefu wa mikopo linalowakabili
wafanyabiashara wengi nchini ili kusaidia uanzishwaji wa viwanda.
Hayo
yamesemwa na Afisa Biashara wa Wizara hiyo Bw. Baruti Mwaigaga wakati
akizungumza katika Viwanja vya Mwl Nyerere wakati wa maonesho ya
Sabasaba yaliyoanza leo jijini Dar es Salaam.
“Kufuatia
kuwepo kwa tatizo kubwa la upatikanaji wa mikopo kwa watu wenye nia ya
kuanzisha viwanda hapa nchini, Serikali imeandaa utaratibu maalumu wa
kutoa taarifa zinazohusu upatikanaji wa mikopo ili kusaidia wananchi,
kitu ambacho hakikuwepo awali” alisema Bw. Mwaigaga
Alisema
lengo la mkakati huo ni kumrahisishia mwananchi mwenye nia ya kuanzisha
kiwanda kupata taarifa sahihi ikiwa ni pamoja na utaratibu mzima wa
kupata mkopo ambao unaondoa usumbufu kwa walengwa ikiwa ni utekelezaji
wa nia ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kuifanya Tanzania kuwa nchi ya
viwanda.
Mikakati
mingine ya Serikali katika kukuza sekta ya viwanda nchini ni pamoja na
kuanzisha programu ya kuendeleza viwanda vidogo vidogo katika mikoa ya
Ruvuma, Pwani, Iringa, Tanga na Manyara.
Naye,
Afisa Uchumi kutoka Wizara hiyo Bw. Vicent Turuka alisema katika
kutekeleza azma ya Serikali ya kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda,
Wizara inawaunganisha wafanyabiasha wadogo wadogo na wanunuzi wakuu na
kuwapatia masoko ya mazao mfano zao la ufuta lina soko kwa kampuni ya
Oramu pamoja na Murza Mills.
Comments
Post a Comment