MAKAMU WA RAIS AHIMIZA AMANI NA UMOJA WAKATI WA TAFRIJA YA FUTARI ILIYOANDALIWA NA BAKWATA
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akizungumza wakati wa tafrija ya Futari iliyoandaliwa na Baraza Kuu la
Waisalm wa Tanzania (Bakwata) iliyofanyika kwenye uwanja wa shule ya
sekondari ya Kinondoni Muslim ambapo alimuwakilisha Mhe. Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na kuwahimiza
viongozi wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) waendelee kuombea
amani katika Taifa na kukemea ipasavyo vitendo vya uhalifu katika jamii
ya Kitanzania.
Mufti
Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeir akizungumza wakati wa tafrija ya
futari iliyoandaliwa na Baraza Kuu la Waislamu wa Tanzania ambapo
alisema uongozi wa sasa wa BAKWATA umedhamiria kudumisha umoja,upendo na
mshikamano baina ya Waislamu wote nchini, Tafrija hiyo ambayo mgeni
rasmi alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.
Samia Suluhu Hassan aliyemuwakilisha Mheshimiwa Rais wa Jamhuri
Muungano wa Tanzania.
Sehemu ya
wageni waliohudhuria tafrija ya futari iliyoandaliwa na Baraza Kuu la
Waislam katika viwanja vya Shule ya Sekondari ya Kinondoni Muslim jijini
Dar es Salaam.
Mwenyekiti
wa Jopo la Masheikh Sheikh Suleiman Amran Kilemile akitafsiri moja ya
aya ya Quran inayojenga na kuimarisha umoja na mshikamano kwa waislam.
Sheikh
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Shekh Alhad Mussa Salum akitoa utambulisho
wa wageni wa jumuiya mbali mbali za waislam waliohudhuria tafrija ya
futari iliyoandaliwa na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania na kuhudhuriwa
na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan.
Viongozi
wa Wanawake Waislamu Tanzania wakisikiliza kwa makini nasaha za
viongozi mara baada ya kufuturu katika tafrija ya futari iliyoandaliwa
na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania.
Chanzo: mjengwablog
Comments
Post a Comment