Taarifa ya uteuzi wa M/Kiti na Wajumbe wa Bodi za TANESCO, STAMICO


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA NISHATI NA MADINI

TAARIFA KWA UMMA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli, amemteua Dkt. Alex L. Kyaruzi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).

Kufuatia uteuzi huo, Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Profesa Sospeter M. Muhongo (Mb.), amewateua wafuatao kuwa Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa TANESCO kuanzia tarehe 31/5/2016 hadi tarehe 30/5/2019;
  1. Dkt. Samwel Nyantahe
  2. Dkt. Lugano Wilson
  3. Bw. David Elias Alal
  4. Mhandisi Stephen Peter Mabada
  5. Mhandisi Leonard R. Masanja
Aidha, Waziri wa Nishati na Madini, Mhe. Profesa Sospeter Muhongo (Mb) amekamilisha uteuzi wa Wajumbe wa Bodi ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), kuanzia tarehe 30/5/2016 hadi 29/5/2019wajumbe hao ni :
  1. Bw. Abdalah H. Musa
  2. Dkt. Coretha Komba
  3. Bw. Felix M. Maagi
  4. Dkt. Lightness Mnzava
  5. Bw. John B. Seka 
Uzinduzi wa Bodi hizo utafanyika Makao Makuu ya Mashiriki hayo Siku ya Alhamisi tarehe 2 Juni, 2016,saa 4:00 asubuhi kwa Bodi ya STAMICO na saa 8:00 mchana kwa Bodi ya TANESCO.

Imetolewa na;
KATIBU MKUU
31 MEI, 2016

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA