Klabu ya soka nchini, Azam FC inayoshiriki ligi kuu soka ya VodaCom Tanzania Bara imetangaza usajili wa wachezaji ishirini na wawili, wanane kati yao wakiwa wapya huku kumi wa kikosi kilichopita wakiachwa. Picture Said Mohammed Abeid / Mwenyekiti - Azam FC Katika taarifa iliyomo katika tovuti ya klabu hiyo, wachezaji wapya waliosajiliwa na timu hiyo ni Mohamed Binslum (Huru), Jackson Chove (JKT Ruvu), Jabir Aziz na Ramadhan Chombo 'Redondo' (Simba), Mrisho Ngasssa (Yanga), Kalimangonga Sam Daniel Ongala Rampling 'Kali Ongala' (GIF-Sweeden), Patrick Mutesa Mafisango (APR- Rwanda) na Peter Senyonjo (Polisi-Uganda). Wachezaji waliobaki ni John Bocco, Erasto Nyoni, Jamal Mnyate, Salum Aboubakar 'Sure Boy', Vladmir Niyonkuru, Philip Alando, Luckson Kakolaki, Malika Ndeule, Aggrey Morice, Salum Swed, Ibrahim Shikanda, Ally Manzi, Seleman Kasim 'Selembe' na Ibrahim Mwaipopo. Wachezaji waliopanda toka timu ya vijana 'Azam Academy' ni sita ambao ni Sino A...