Anaswa akimlawiti mtoto wake Liveee!!

Watoto wa kazi wa Afande Mwema,mkoani Pwani limemtundika nyuma ya nondo mpuuzi mmoja aliyetambulika Ally Salehe (36), mkazi wa Kibaha, kwa tuhuma za kukutwa akimlawiti mtoto wake wa kiume ambaye ni denti wa darasa la nne.

Kwa mujibu wa bosi wa Polisi mkoani Pwani, Absalomon Mwakyoma, mtuhumiwa huyo alikamatwa juzi usiku baada ya kukutwa na majirani akifanya kitendo hicho cha kinyama.

Amesema majirani walikuwa na tetesi kuhusiana na mtuhumiwa kumfanyia kitendo hicho mtoto huyo ambaye ni wa mkewe lakini walishindwa kumchukulia hatua.

Amesema siku za mwizi ni arobaini kwani mtuhumiwa alikuwa akifanya kitendo hicho kwa muda mrefu hivyo juzi usiku majirani walimnasa live mtuhumiwa akimfanyia ukatili mtoto huyo pembeni ya mti karibu na nyumba wanayoishi.

Baada ya majirani kumkamata mtuhumiwa huyo walianza kumpa kipigo kikali na kisha kumpeleka kituoni.

Imedaiwa wakati mtuhumiwa huyo anafanya kitendo hicho mkewe alikuwa ndani akiendelea na shughuli nyingine.

Hata hivyo imedaiwa kuwa mke wa mtuhumiwa huyo alikuwa akifahamu kitendo alichokuwa akimfanyia mtoto wake kwa kipindi kirefu lakini aliogopa kumuuliza kwa kuhofia ndoa yake kuvunjika.

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA