Serikali kudhibiti wizi wa pamba Bunda

SERIKALI imesema katika msimu wa ununuzi wa zao la pamba ujao wa mwaka 2011, itaagiza mizani ya kisasa, ili kudhibiti udanganyifu kutoka kwa wafanyabiashara wa zao hilo ambao wamekuwa wakipunja wakulima kwa kutumia mizani ambayo haina ubora.

Pia katika msimu ujao serikali itazikusanya mizani yote ya sasa kutoka kwa wanunuzi hao wa zao la pamba, ili zisitumiwe tena katika kupimia zao hilo.

Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Stephen Wassira, alieleza hayo mwishoni mwa wiki katika Kijiji cha Kung’ombe wilayani hapa wakati akizungumza na wananchi kwenye mkutano wa kampeni za kuwania kuteuliwa kwenye kura za maoni za wananchama wa CCM katika Jimbo la Bunda.

Alieleza hayo baada ya kuulizwa na mwananchi kuhoji serikali imejipanga vipi katika kukabiliana na tatizo la wanunuzi wa zao la pamba wanaotumia mizani mibovu kwa lengo la kuwapunja wakulima.

Akijibu swali hilo, Wassira alisema serikali imeweka mipango madhubuti wa kuhakikisha wakulima wa zao la pamba hawafanyiwi udanganyifu wa aina yoyote na wanunuzi wa zao hilo kwa kutumia mizani mibovu.

Alisema katika msimu ujao serikali itanunua mizani mipya ambayo ni ya kisasa aina ya digital ambayo itakuwa inaonyesha hali halisi ya uzito wa pamba pamoja na kuonyesha hali ya hatari kama mnunuzi anataka kufanya udanganyifu wowote pindi anapopima pamba ya mkulima.

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA