Posts
Showing posts from March, 2012
SHOW YA DIAMONDS ARE FOREVER YAFUNIKA VIIBAYA VIBAYA MNOOOOO.
- Get link
- X
- Other Apps
DJ Bulla mtamboni akihakikisha show ya Diamond inakwenda sawa kabisa. Huyu jamaa bwana ni bonge la design wa mavazi, nguo unazoona alizovaa Diamond na wakina Barnaba, Ommy Dimpozi na Amini huyu ndio aliyechora mpango mzima utakavyokuwa. Anaitwa Martin Kadinda Anaitwa Esi yeye alikuwa akishughulika na usafi wa Diamond na kuonekana kwa steji kweli kamweka sawa raisi wa Wasafi DIAMONDS ARE FOREVER RED CARPET @Mlimani City Dar es Salaam Hapa ndipo palipokuwa sehemu ya wageni wote kupiga picha kabla yakuingia ukumbini, nimependa mwonekano ulivyokuwa umekaa, big up kwa waandaaji. PICHA ZOTE NA STORY NI KUTOKA KWA DJCHOKA
TIMU YA PUBLIC RELATIONS (PR2) YATINGA ROBO FAINALI YA FAWASCO KWA KISHINDO
- Get link
- X
- Other Apps
Hatimaye leo katika kiwanja cha Nyegezi Seminary, timu ya PR2 imeweza kuonyesha uwezo wake wa kusakata soka baada ya kuichapa Timu ya Baso2 goli 1-0 na kuweza kuingia Robo fainali.Timu ya PR 2 imekuwa ikakabiliwa na mizegwe mbalimbali pindi wawapo viwanjani hasa pale wachezaji wake mahili wanapopigwa kadi Nyekundu na hivyo kukosa michezo muhimu kama wa leo. "kila siku sisi tu kuonewa wachezaji wetu wamekuwa wakichezewa vibaya mara kwa mara lakini Refa anapeta tu”amekaliliwa mmoja wa mashabiki kutoka PR. Blog hii imeweza kufanya mahojiano na baadhi ya wachezaji wa timu ya PR kuwa safari hii wamejipanga sana kwa michezo yote iliyobaki na watajitahidi kadri ya uwezo wao na kuhakikisha kuwa safari ya kwenda Kagame ni ya kwao,na mamillion yote yanayotolewa na chuo cha Mt.Augustino katika mashindano haya ya FAWASCO yanabaki mikononi mwao. Angalia na video baada ya mechi pamoja na picha zilizochukuliwa baada ya ushindi…japokuwa hazikuwa katika ubora wa kutosha.
MIKAKATI YA KUWEKA MANISPAA YA MUSOMA SAFI YAZIDI KUBOREKA
- Get link
- X
- Other Apps
Manispaa ya Musoma Mkoa wa Mara imejiwekea malengo ya kufanya usafi wa mazingira kila Ijumaa ya mwisho wa mwezi ili kuweka mji huo katika hali ya usafi. Akisoma Risala siku ya uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya usafi wa mazingira, Afisa Afya wa Manispaa hiyo, Peter Mtaki alisema kuwa uzinduzi huo utakuwa chachu uya uendeshaji wa usafi wa mazingira kwa kila mtu, kaya, nyumba, mtaa na kata. “Pia kampeni hii itafanya watu wabadili tabia na kuona kuwa suala la usafi si la watumishi wa Idara ya Afya pekee ni suala la mtambuka kila mtu kwenye eneo lake analoishi na anakofanyia kazi mazingira yake yawe safi,” alisema Mtaki. Alisema kuwa halmashauri hiyo lishatunga sheria ndogo ya usafi wa mazingira ambayo mpaka sasa ndiyo inayotumika ambapo sheria hii inamtaka kila mkazi kuweka eneo lake safi kuanzia majumban, eneo lake la kazi na maeneo ya biashara pamoja na kuchangia kiasi cha shilingi 500kama ada ya usafi. Vile vile halmashauri ilianza kuunda vikundi vya usafi katik
ZAMARAD AMSHUKURU MUNGU BAADA YA KUJIFUNGUA SALAMA
- Get link
- X
- Other Apps
Mtangazaji wa Kipindi cha TAKE ONE cha Clouds TV, Zamaradi Mketema juzikati alijifungua mtoto wa kiume katika Hospitali ya Aga Khan na kumshukuru Mungu kwa kuutua mzigo huo salama. Akichonga na mpekuzi wetu hivi karibuni jijini Dar, Zamaradi alisema kipindi chote cha ujauzito wake kuna waliodhani angejifungua kwa operesheni lakini Mungu amekuwa upande wake. “Nina kila sababu ya kumshukuru Mungu kuniwezesha kujifungua salama kwa njia ya kawaida. Nafurahi kumpata mtoto huyu wa kiume na huu ni mwanzo wa maisha mapya, ” alisema Zamaradi. Mtangazaji huyo amejifungua zikiwa zimebaki siku chache kwa wasanii wa filamu Ndumbagwe Misayo ‘Thea’ na Shamsa Ford nao wajifungue.
DJ ZERO KUWAKILISHA USHINDANI KATI YA MA-DJ WA REDIO NA MA-DJ WA CLUB KATIKA USIKU WA REDDS LIPS CLUB MWANZA
- Get link
- X
- Other Apps
BAADA YA MGOMO HATIMAYE DALADALA ZAREJEA KUTOA HUDUMA.
- Get link
- X
- Other Apps
Mbunge wa Nyamagana Ezekiel Wenje akizungumza na madereva hao kuwasihi kurejea katika huduma kwani wananchi wanataabika. Kamanda wa jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza Liberatus Barlow akiwataka madereva hao kurudi katika huduma kwani suala lao tayari limekwishafika katika vyombo husika. Wakati huo huo Mwenyekiti wa chama cha madereva wa daladala Kanda ya Ziwa Protas Dede, amewaomba radhi wananchi kwa hali iliyotokeza na usumbufu walioupata kwani imewabidi kuchukuwa hatua hiyo kwa dhamira ya kutetea haki yao ili mambo yaende sawa. Dereva wa daladala akitoboa kero zake mbele ya wanausalama barabarani. Sasa ni zamu ya mwanausalama.. Mwisho ikawa ligi... Hivi ndivyo hali ilivyokuwa huku jeshi la polisi likiimarisha ulinzi eneo la kusanyiko viwanja vya Ghand Hall jijini Mwanza. Usalama uliimarishwa kama kawa.. Haikujulikana ni nini kilikuwa kimewasibu wanafunzi hawa hata wakafungwa pingu za kamba wakielekea kituo cha polisi kati. picha na story nzima ni kutoka www.gsen