LIONEL MESSI AWEKA HISTORIA KWENYE KLABU YA BARCELONA

MUARGENTINA Lionel Messi sasa ndiye mfungaji bora wa kihistoria wa Barcelona. Mshambuliaji huyo ameweka jina lake katika historia za kudumu za klabu hiyo baada ya usiku huu kupiga mabao matatu peke yake na kutimiza mabao 234 hivyo mfungaji nambari moja milele wa klabu hiyo. “Tuko nyuma ya mchezaji bora hakika kwa kila namna,” alisema kocha wa Barcelona, Pep Guardiola. “Anastahili kwa kila kitu ambacho mwanasoka anatakiwa kufanya na amefanya hivyo kila baada ya siku tatu. Messi alifunga hat trick yake ya 18 kihistoria akiwa na klabu hiyo ya Catalan na kuvunja rekodi ya gwiji wa klabu hiyo, Cesar Rodriguez aliyefunga jumla ya mabao 232 iliyodumu kwa miaka 57, na kuingia kwenye orodha ya magwiji wa kihistoria waliofanya mambo makubwa kwenye Uwanja wa Camp Nou. Wakati Cesar aliweka rekodi hiyo ndani ya miaka 13 kuanzia msimu wa 1942 hadi 1955, kijana huyo mwenye umri wa miaka 24, Messi amehitaji misimu minane tu kufa nya mambo hayo adimu. Messi alifunga mabao hayo katika ushindi wa kwenye mechi ngumu kuliko ilivyotarajiwa wa mabao 5-3 dhidi ya Granada, mechi ambayo timu yake ilikuwa lazima ishinde kama inataka kuweka hai matumaini ya kutwaa taji la nne mfululizo la Ligi Kuu ya Hispania, La Liga. Muargentina huyo aliunganisha krosi ya Isaac Cuenca dakika ya 17 na kufikia rekodi ya Cesar, na kasha akapiga mawili zaidi kwa pasi za Dani Alves kuipatia ushindi timu yake, baada ya Granada kusawazisha na kupata 2-2. Messi, mwanasoka bora wa dunia mara tatu, sasa amefikisha mabao 54 kwenye mashindano yote msimu huu, yakiwemo ya rekodi katika mechi moja ya Ligi ya Mabingwa, matano wiki mbili zilizopita. Wakati wote safu ya ulinzi ya wapinzani huwa na mchecheto juu yake, Messi amethibitisha yeye hazuiliki, akifunga mabao 17 katika mechi saba mfululizo. Hat trick yake katika mechi na Granada inamfanya sasa awe anaongoza kwa mabao kwenye La Liga, akimzidi mawili mpinzani wake mkubwa, Cristiano Ronaldo wa Real Madrid. Ushindi huo wa sita mfululizo kwa Barcelona, unapunguza idadi ya pointi ambazo wanazodiwa na vinara wa La Liga, Real Madrid hadi kubaki tano, ingawa wapinzani wao Jumatano hii wanashuka dimbani na Villarreal. Barcelona awali ilikuwa inaamini kwamba Cesar amefunga mabao 235 ndania ya misimu 13 kati ya 1942 na 1955, lakini baada ya kurudia kupitia makabrasha yan historian a rekodi kwa pamoja na gazeti la La Vanguardia, wakagundua walimuongezea Cesar mabao matatu. Messi amefunga mabao 153 katika ligi ya Hispania, 49 katika Ligi ya Mabingwa, 19 katika Kombe la Mfalme, nane katika Super Cup ya Hispania, manne katika Klabu Bingwa ya Dunia na moja kwenye Super Cup ya Ulaya.

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA