SSPRA WATEMBELEA HIFADHI YA SERENGETI
Wanachama wa SSPRA mwishoni mwa wiki iliyopita siku ya Ijumaa tarehe 16/03/2012,kuanzia majira ya saa 2 asubuhi walianza safari yao ya kuelekea katika hifadhi ya taifa ya Serengeti (SENAPA) Katika kujifunza mambo mbalimbali yanayoendana na taaluma wanayosomea ya Uhusiano wa Umma na Masoko.(Public Relations and Marketing),pia katika kuendeleza sera ya utalii wa ndani ambayo imekuwa ukilegalega sana hapa nchini.
Safari hii imekuwa yenye mafanikio makubwa sana kwani kila kitu kilichokuwa kimepangiliwa na kamati ya Mafunzo ya nje kwa vitendo chini ya Mwenyekiti Bw.Mshana Shaabani imeweza
kutekelezeka vizuri sana . Wanachama wameweza kujifunza mambo mengi
sana ambayo hawakuwa wakiyafahamu kutoka kwa Afsa utalii Bw. Fred Shirima
kama vile historia halisi ya Serengeti,umuhimu wa hifadhi ya Serengeti
kwa Tanzania na dunia nzima,sifa za hifadhi ya Serengeti iliyonayo,
vivutio vya kipekee vinavyopatikana katika hifadhi hii pekee, na pia
changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo katika utendaji wa kazi za
uhifadhi. Pia Bw. Sadati Kimaro ambaye alikuwa ni
mwongozaji wa safari (game driver) wakati wote ndani ya hifadhi alitoa
maelezo mbalimbali yanayohusiana na wanyama hakuchoka kujibu maswali
yote pindi alipokuwa akiulizwa na wanachama wa SSPRA.
Uongozi wa SSPRA unapenda kutoa shukrani zake za dhati kabisa kwa Uongozi wa hifadhi ya Taifa ya Serengeti kwa
kuitikia ombi la SSPRA, Uongozi wa chuo kikuu cha Mt.Augustino kupitia
idara ya uhusiano wa umma chini ya mkuu wa idara Cezalia B. Mwidima,
wadhamini wa safari kampuni ya SBC Company Limited (Pepsi), Mukeshi travels, pia mlezi wa SSPRA Bw.Albert Tibaijuka.
Zifuatazo ni baadhi ya picha zilizochukuliwa wakati wa safari,pia Video itakuwepo baada ya kumaliza kuifanyia editing.






































































Good job SSPRA n that how the PR should be,tumeusahau utalii wa ndani kwa muda mrefu...vivutio ni kwa ajili yetu sio wazungu pekee yao!!
ReplyDelete