Airtel yaja na internet ya 3.75G kutoa ubora na kasi zaidi kwa wateja.

Meneja Masoko wa Airtel Bw Salim Madati akitoa ufafanuzi kwa waandishi
wa habari juu ya huduma mpya ya 3.75G katikati uzinduzi uliofanyika
leo katika makao makuu ya Airtel Morocco ambapo sasa wateja wa Airtel
wataweza kupata huduma ya internet iliyo ya kasi na kuwapatia ufanisi
Zaidi katika shughuli zao za kila siku.
Airtel Marketing manager Salim Madati explicate on 3.75G data service
to the press during the launch of 3.75G mobile platform in the
country, which promises to change how subscribers experience the web
on internet-enabled cell phones. The launch ceremony held at Airtel
headquarter Morocco and attended by members of press 

Mkurugenzi mkuu wa Airtel Bw Sam Elangallor akionyesha jinsi gani
huduma ya 3.75 inavyoweza kutoa huduma ya internet iliyo ya kasi na
kuwawezesha wateja wa Airtel kufanya video call wakati wa  uzinduzi wa
huduma ya 3.75 iliyofanyika makao makuu ya Airtel na kuhudhuriwa na
waandishi wa habari , wakishuhudia (kulia) ni mkurungezi wa
mawasiliano wa Airtel Bi Beatrice Singano Mallya na (kushoto )ni
Meneja masoko Salim Madati.
Airtel Managing Director Sam Elangalloor reveal 3.75G technology which
will enhance multimedia functionality, high speed mobile broadband and
internet access; allowing  Airtel Customers  to make video calls,
watch live TV, send and receive emails, and download music from the
handheld devices. During 3.75G  launch ceremony held at Airtel
Headquarters and attended by media on the (left) Airtel communication
Director Beatrice Singano Mallya and Marketing Manager Salim Madati 

Mkurugenzi mkuu wa Airtel Bw Sam Elangallor akiongea na waandishi wa
habari (hawapo pichani) wakati wa halfa fupi ya  uzinduzi wa huduma ya
3.75G  ambayo itatoa huduma ya internet yenye ubora na kasi zaidi  kwa
watumiaji wenye simu zenye uwezo wa kutumia internet wawapo mahali
popote. Uzinduzi huu ulifanyika katika makao makuu ya Airtel morocco
Airtel Managing Director Sam Elangalloor reveal 3.75G address the
member of press (not in picture) during the 3.75G service that will
provide high speed mobile broadband and internet access and allowing
Airtel customer use fast internet service anywhere in the country. 

Mkurugenzi mkuu wa Airtel Bw Sam Elangallor na mkurungezi wa
mawasiliano wa Airtel Bi Beatrice Singano Mallya  kwa pamoja
wakionyesha jinsi gani huduma ya 3.75G  ilinavyoweza kuwawezesha
wateja wa Airtel kupata huduma ya internet yenye ubora na kasi zaidi
kwa watumiaji wenye simu zenye uwezo wa kutumia internet ikiwa ni
pamoja na  kufanya video call wakati wa halfa fupi ya uzinduzi wa
3.75G  iliyofanyika makao makuu ya Airtel Morocco.
Airtel Managing Director Sam Elangalloor and Airtel communication
Director Beatrice Singano Mallya jointly demonstrate how 3.75G
capability will allow Airtel customers to make video calls, watch live
TV, send and receive emails and download music from their cellular
phones, this occurred  during the launch held at Airtel Headquarters
Morocco 

Mkurugenzi wa Airtel Sam Elangallor akiinua modem na kumkabidhi
Mwandishi wa habari kutoka TBC Jane John aliyejishindia modem wakati
wa uzinduzi wa huduma ya 3.75G iliyofanyika makao makuu ya Airtel na
kuhudhuriwa na waandishi wa habari, wakishuhudia ni baadhi ya
wafanyakazi wa Airtel
Airtel Managing Director Sam Elangalloor handover a modem to TBC news
reporter Jane John who won herself a modem during  Airtel 3.75G launch
ceremony held at Airtel headquarters and attended by members of press,
in the picture are Airtel staff  representatives 

Mkurugenzi wa Mawasiliano Airtel Bi Beatrice Singano Mallya akiongea
wakati wa uzinduzi wa huduma ya 3.75G uliofanyika leo katika makao
makuu ya Airtel Morocco ambapo sasa wateja wa Airtel watapata internet
yenye ubora na kasi  zaidi  , Pichani ni Mkurugenzi wa Airtel Sam
Elangallor

Airtel yaja na internet ya 3.75G kutoa ubora na kasi zaidi kwa wateja.
•    Airtel yajenga mtandao bora wa data barani Afrika
•    Uzinduzi wa Airtel 3.75G Tanzania utawapatia watumiaji  wa data
huduma yenye kasi na ubora zaidi  katika simu zao
•    Kupitia internet ya 3.75 itawawezesha wateja kufanya maongezi ya
simu ukiwa unamwona mtu, kuangalia TV, kutuma na kupokea barua pepe na
kuperuzi na kupata miziki kutoka kwenye tovuti kupitia simu zao.
Jumanne 13 Machi 2011, Dar es Saalam–Airtel Tanzania leo imepiga hatua
kubwa katika kujenga na kukuza mtandao wa technoloijia ya 3.75G Africa
kwa  kuzindua rasmi  mtambo wa 3.75G nchini Tanzania,ambapo Airtel
itatoa huduma ya internet yenye ubora na kasi zaidi  kwa watumiaji
wenye simu zenye uwezo wa kutumia internet wawapo mahali popote.
Mkurungenzi Mkuu wa Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Sam
Elangalloor alieleza” kukua kwa technolojia hii kutakuza ufanisi
katika vyombo mbalimbali vya  mawasiliano (multimedia), kwa kuwa 3.75G
itatoa internet yenye ubora na kasi  zaidi kwa  kuwezesha wateja
kufungua tovuti mbalimbali, kufanya maongezi  ya simu kwa njia ya
video , kuangalia TV, kutuma na kupokea barua pepe na pia  kupata
muziki kutoka kwenye tovuti  kwa kutumia simu
Teknologia ya 3.75G itatoa nafasi kwa wateja kupata mawasiliano ya
data kwa njia tofauti na ya pekee kabisa, ndio maana leo Airtel
tunajisikia fahari kuwa internet yetu ya 3.75G ni uvumbuzi na
muendelezo wa mtandao (platform) wetu ili kuwawezesha wateja wa Airtel
wote nchini kupata huduma ya internet au data yenye ubora wa hali ya
juu pamoja na kasi zaidi”
Tunafanya ubunifu wa kuleta huduma zenye ubora zaidi katika mtandao
kwa kuzingatia kuwa sasaivi dunia inauhitaji mkubwa sana wa huduma za
kimtandao hasa kupitia simu ya mkononi
Ukirejea takwimu zilizofanywa na kampuni ya McKinsey & Co.
Telecommunications zinaonyesha  mpaka sasa kuna watumiaji wa simu za
mkononi wapatao milioni 400 Afrika, na kwamba bara la  Afrika ni moja
kati ya  soko linalokuwa kwa kasi zaidi huku soko la simu za mkononi
likiendelea kukua na kupanuka zaidi na kufikia kutoa huduma za
internet, huduma za benki kwa njia simu (mobile banking)  na biashara
kwa njia ya mtandao yaani (mobile commerce) .

Hivyo basi kwa kuzingatia hili,  ndio maana Airtel tunaendelea na
mikakati kama hii ya kuwaletea wateja internet yenye kasi zaidi ya
3.75G ambayo ni sambamba  na lengo letu la kuendea kupanua mtandao
ili kutoa mwanya wa mawasiliano kuwafikia wakazi wengi wa vijijini
ambao walikuwa wamesahaulika na mapinduzi ya mawasiliano katika bara
la Afrika.
“wote tunafahamu kuwa mawasiliano ni nyenzo muhimu kwa maendeleo ya
jamii ya sasa lakini bado kunachangamoto kubwa sana katika kupata
huduma hii kwa baadhi ya sehemu barani Africa. Lakini tukumbuke
Mawasiliano ni haki ya msingi kwa kila mtu na si vinginevyo hivyo kwa
kupitia mtandao wa Airtel internet yenye kasi zaidi ya 3.75G ninaamini
tutaweza  kuunganisha idadi kubwa ya watu kwa kukuza mahusiano ndani
na nje ya ya jamii zetu, kuendeleza na kuutangaza utamaduni wetu,
pamoja na kupanua wigo wa wale wanaofanya biashara kupitia mtandao wa
internet “ Aliongeza Elangalloor.
Ikiwa tayari mteja ameunganishwa na teknologia ya 3.75G simu yake
itaonyesha 3.75G, HSDPA, WCDMA or HSPA. Hii inategemeana  na Aina ya
simu aliyonayo mtumiaji lakini kasi ya kuunganishwa ni yenye ubora
zaidi.
Airtel itaendelea kuwekeza kwenye huduma ya data katika soko lake lote
huku lengo likiwa ni kuwa mtandao mpana zaidi wa teknologia ya 3.75G
katika bara zima, na itaendelea kutoa huduma bora na inayokidhi
mahitaji ya watumiaji

- Ends-

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA