FAIDA TANO ZA KUMBUSU MWENZI WAKO ‘DEEP KISS’, KIAFYA, KIMAPENZI NA TAHADHARI WAKATI WA KUBUSU #PoweredBy VICTORIA THERAPIES

JIUNGE NA UKURASA WA VICTORIA THERAPIES WA FACEBOOK KUPATA TAARIFA ZOTE KUHUSU TIBA MBADALA NA USHAURI WA KIMAHUSIANO BOFYA HAPA KU LIKE PAGE YA FACEBOOK

1. Husaidia kuiboresha afya yako 
Unampombusu mkeo au mmeo kwa moyo wote na hisia zote (hapa tunaongelea deep kiss ‘kula den*a’) unapata faida kubwa kiafya ambao kitaalam tendo hilo huweza kusaidia kukupunguzia maumivu ya kichwa kwa kupumzisha taratibu misuli. Pia kitaalam tendo la busu hukusaidia kuing’arisha ngozi yako kama inavyofanyika kwa mtu anaependa mazoezi. Hivyo basi unapotaka kulala, ni vyema ukambusu kwa hisia mkeo/mmeo upate faida hizi badala ya kumpotezea na kumrukia wakati wa tendo la ndoa.

2. Husaidia katika ufanyaji kazi wa virutibisho mwilini
Inaelezwa kuwa busu husaidia sana mwili kufanya mrejesho ambao unadhibiti ufanyaji kazi wa virutubisho mbalimbali mwilini hivyo inaweza kusaidia katika kuboresha afya yako zaidi.

3. Busu huongeza furaha na kupunguza msongo wa mawazo.
Kwa mujibu wa tafiti mbalimbali zilizofanywa inaelezwa kuwa tendo la busu huongeza kitu kinachojulikana kama ‘endorphins’, na endorphins husababisha mtu afurahi. Kama hivyo ndivyo, kwa nini usiitafute furaha kwa mwenzi wako kwa njia mojawapo ya kujisikia raha kwa kumbusu tu.
Sio hivyo tu lakini pia busu husaidia kupunguza msongo wa mawazo. Unapoongeza furaha, unapotuliza akili na kuachia hisia zako kwa tendo la busu unapunguza kwa kiasi kikubwa msongo wa mawazo ambao ni chanzo cha magonjwa mengi.

4. Busu huongeza hamu ya kufanya tendo la ndoa
Moja kati ya mambo ambayo yanaweza kuwasaidia wanandoa kujiandaa kwa pamoja na kupata hamu ya tendo la ndoa zaidi ni busu. Hii ni kwa sababu tendo hili hufanywa kwa pamoja na wawili hao huku kila mmoja akivuta hisia kwa nguvu asiyoifahamu.
Mtaalam mmoja wa masuala ya uhusiano aliwahi kutaja ‘busu’ kama tendo linaloongeza mihemko zaidi ya tendo lolote la kisaatabu wakati wa maandalizi ya tendo la ndoa.

5. Busu hujenga mapenzi zaidi, huongeza mapenzi ya dhati
Tendo la busu huwafanya wanandoa kuwa katika hali ya umoja zaidi kihisia. Hali hiyo huwaongezea upendo moyoni kwa kuwa tendo hilo huongea zaidi ya maneno na ndio maana wakati wa tendo hilo ukimya hutawala na hisia huongea zaidi.
Profesa Mmoja aitwae Dawn Maslar aliwahi kusema kuwa ‘tunawabusu tunaowapenda, na tunawapenda tunaowabusu’. Mbusu mkeo/mmeo kwa dhati uwe katika nafasi ya kuongeza na kuimarisha mapenzi yenu.

Hata hivyo, unapaswa kuchukua tahadhari na kuwa na busara pale unapotaka kufanya tendo la busu na mwenzi wako kwa kuwa tendo hili kwa utamaduni wa kiafrika huhitaji ‘faragha’ na huleta ukakasi linapofanyika hadharani.

Kumbuka ni muhimu sana kuwa mwaminifu kwa mtu unaembusu, mbusu mwenzi wako pekee kwa kuwa kuna magonjwa mengi yanayosambaa kutokana na tendo hili vikiwemo virusi vya ukimwi. Mshauri mwenzi wako atunze vyema kinywa chake kwa kuzingatia kusugua meno kwa usahihi kila baada ya kula.

Kumbuka kufika VICTORIA THERAPIES, MTONI KIJICHI, TEMEKE, DAR ES SALAAM kupata tiba ya sahihi ya magonjwa mbalimbali na ushauri wa kina. Kuwa huru na maisha yenye afya njema.

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA