JINSI YA KUKABILIANA NA MATATIZO KATIKA MAHUSIANO POWERED BY VICTORIA THERAPIES


ENDELEA KU LIKE UKURASA WA FACEBOOK WA VICTORIA THERAPIES KUPATA TAARIFA ZAIDI KUHUSU MAHUSIANO NA TIBA MBADALA  BOFYA HAPA


Katika mahusiano kuna Sababu nyingi zinazopelekea watu kuwa na migogoro mara kwa mara. 

Tutawawaletea vyanzo hivyo katika ukurasa huu, na moja kati ya vyanzo hivyo ni pamoja na kutokujua tabia za wenza wetu.
Katika mada ya leo tutajikita zaidi katika sababu ya ‘Tabia’.
Tuanze kwa kuzifahamu aina kuu nne za tabia za binadamu..

Kwa kawaida Binadamu tupo katika makundi makuu manne ya tabia kuu ambazo watu wengi wamo.
Kwa hali hiyo ni vema ukafahamu makundi hayo ili uweze kujua mpenzi wako yupo katika kundi lipi hali itakayokusaidia kuishi kwa amani kwani ukishamfahamu mtu tabia yake hatakupa shida kuishi nae.

KUNDI LA KWANZA

SANGWINI
• Watu wa kundi hili mara nyingi ni watu wachangamfu,
• Wenye mikasa mikasa inayofurahisha,
• Wana jiamini sana,
• Wenye matarajio makubwa katika kila kitu,
• Wakunjufu wa mioyo na niwatu wenye huruma
• Kila wanapokuwepo wanauwezo wa kupata marafiki wengi
• Akiwa ni mshauri basi watu wake watafarijika na kuridhika sana
• Kama ni muuguzi basi hutoa maneno ya kufariji sana na kuleta nafuu na faraja kwa mgonjwa
• Wanakubalika na watu wana uwezo wa kuwa wanasiasa wazuri
• Kama ni Mwalimu huwa ni Mwalimu mzuri lakini hamalizi silabasi kwa kutoa mifano mingi
• Katika mapenzi wana ashki kali hupenda sana KUHONDOMOL

Mapungufu ya Sangwini
• Anaweza akasema tu jambo bila kufikiri
• Hutekeleza mambo kijujuu tu hawayachukulii mambo kwa upana au kwa kina
• Hawatunzi ahadi na maneno yao si ya kuyaamini sana
• Hupoteza marafiki kwa haraka kwani kwake si shida kupata au kutengeneza marafiki wapya
• Sio mtunza siri mzuri hapendi kuweka mambo moyoni mwake

KUNDI LA PILI (MELANCHOLIC)
Melankoliki tabia zao
• Kundi hili ni la mtu mkimya
• Anayachukulia mambo kwa umakini,upana na tahadhari kubwa
• Wana hulka ya kufikiri sana na akili sana
• Watu waaminifu
• Wanajua kutunza siri
• Wanabidii sana katika kazi
• Hufanya bidii kufikia malengo

Mapungufu ya Melankoliki
• Ni watu wenye hasira kali inayudumu kwa muda mrefu
• Hujihisi wadhaifu nasi watu wa kujipa moyo
• Wana hasira za woga
• Huamini mabaya yatawatokea
• Sio wepesi wa kusamehe
• Ni vigumu sana kuishi nao
• Katika mapenzi ashki zao hupanda pole pole

KUNDI LA TATU CHORELIC
Koreliki tabia zao
• Wepesi wa kutenda jambo,kujifunza vitu
• Kuanzisha ufahamu upya
• Wana matarajio makubwa kufikia mafanikio
• Hupenda mambo yaende na anakua mstari wa mbele kutenda mambo ili yaende kama yalivyopangwa
• Hutafuta kwa bidii mafanikio,utajiri na hadhi
• Wana nguvu ya mwili
• Wachapa kazi
• Watawala wa kuzaliwa hana tafadhali
• Hapendi kuona mtu akionewa

Mapungufu yao
• Wana hasira za haraka
• Sio wavumilivu kwa wenzi wao
• Hawana marafiki wengi kutokana na jinsi walivyo
• Mgumu kuomba msamaha
• Na ni mkosoaji anayeweza kupinga mambo hadharani
• Katika mapenzi hawakusemwa sasa kama yumo humu aje atuelezee yukoje katika tendo ashki kali au kati kwa kati au hakuna kitu kabisa

KUNDI LA NNE PHLEGMATIC
Tabia zao Flegmatiki
• Wapole
• Hawakasiriki haraka
• Hupenda Amani mara zote
• Unaweza kumpeleka kokote kirahisi
• Hulka yao ni kumtuliza kila mtu
• Hawapendi kuona mtu kachukia
• Hawapendi kumuudhi mtu
• Ni rafiki wa kila mtu hapendi mapambano
• Daima wao husimamia haki ya kweli
• Katika mapenzi wao kila kitu NDOHO TAABU

Mapungufu yao
• Hufanya mambo bila umakini
• Wanafanya kwa ulegevu unaweza kuwaita ni wazembe
• Hupenda kulala sana
• Hapendi kupinga mambo au kukosoa mapungufu yaliyojitokeza
• Hawapendi migogoro

2.Fahamu tabia yake
• Kiasili mwanaume ni mtawala ili ukae nae kwa usalama lazima ujue hilo na ukubaliane nalo hapo utafanikiwa
• Tambua mambo anayopenda na mambo asiyoyapenda
3.Bakia katika jinsia yako
• Kiasili kila jinsia ina mambo yake ya kiasili sasa ukitaka kutoka katika jinsia yako kitabia na kwenda katika jinsia ya mwenzako lazima mtapata matatizo ni vema ubaki katika jinsia yako
• Tenda kama Mume au Mke
• Ongea kama Mke au Mume
• Wajibika kama Mke au Mume

4.Tambua haki zake na Haki zako
Matatizo mengi hutokea kwa watu kutokujua haki za msingi zao na wenzi wao katika ndoa ikiwemo haki ya tendon a kuridhishwa katika hilo, kupendwa, kusikilizwa, kushirikishwa n.k

5.Timiza Wajibu wako
Haki huendana na wajibu moja kwa moja, wakati unawaza kuhusu haki zako kutoka kwake, hakikisha unatimiza kwa kiwango kinachoridhisha wajibu wako kama mume au mke.
6.Mfunze bila kuwa Mfunzaji
Unapomfunza mkeo usigeuke kuwa mwalimu kama Yule wa darasani. Mfunze taratibu kadri muishivyo kwa upendo kwa kumuelekeza na kumwambia pale alipokosea kwa kutumia mbinu nzuri isiyokera au kukwaza.

Usiwe wewe ndiye mkufunzi tu, mmpe nafasi nay eye akuelekeze kwa kumuuliza mtazamo wake katika uamuzi unaotaka kuuchukua. Muulize pale unapopata utata kwa kumuamini kama mtu anaeweza kutatua tatizo lako kwa mawazo au kutekeleza. Usijikwaze kwake na usithubutu kumdharau.

Tufikie VICTORIA THERAPIES, Mtoni Kijichi, Dar es Salaam kwa ushauri zaidi, na matibabu ya magonjwa sugu na magonjwa yanayotokana na mfumo wa uzazi.
kwa maswali na ufafanuzi zaidi piga 0658027027

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA