DIAMOND PLATNUMZ KUJENGA VISIMA VYA MAJI SAFI KWA SHULE ZOTE ZA TANDALE.

Msanii Diamond Platnumz kupitia kipindi cha XXL, ameudhibitishia umma kuwa ana mpango wa kujenga visima vya maji safi kwa shule zote zinazopatikana katika kata ya Tandale pamoja na madawati, Tandale ndio  sehemu ambaye mkali huyu wa mdogo mdogo amekulia na kusomea.

"Utaratibu wa kuisaidia jamii nimekuwa nikiufanya kwa nyakati tofauti na wakati mwingine kufanya kimya kimya kuepuka zile lawama za kuonekana kujionyesha" Diamond alimjibu Adam Mchomvu ambaye alimuuliza swali kabla ya kumaliza kipindi kama anautaratibu wa kuisaidia jamii yake?  "Ilikuwa afanye kwa siri lakini inabidi aweke wazi tu nishatuma watu wangu kupita kila shule na kujua mahitaji yao, lakini kwa kuanza nina mpango wa kujenga visima vya maji safi kwa kila shule iliyopo tandale na ni kwa gharama yangu mwenyewe".


Interview ya leo kupitia XXL asilimia 90 imezungumzia swala la mahusiano yake na beautiful Onyenye wa Bongo Wema Sepetu, kwa habari zilizopo mtaani ni kwamba wawili hawa  hawapo tena katika mahusino, Diamond kabanwa maswali mengi kama ni kweli wameachana lakini jibu alilokuwa akilitoa ni juu ya wimbo wake huu mpya wa  sasa "nitampata wapi" una majibu yote yaani  A na B, hivyo ni jukumu la msikilizaji mwenyewe kupembua akili. alipobanwa zaidi aweke wazi Diamond alisema muda utakapofika basi kila kitu kitakuwa wazi, 

Inasemekana chanzo cha penzi hili kuingia dosari ni wakati wa birthday ya Wema Sepetu pale Meneja wake Martin Kadinda alipotoa zawadi ya gari lenye thamani kubwa kuliko uwezo wake, Diamond alipoulizwa kuhusu je hicho ndio kimekua chanzo? kama kawaida hakuwa wazi kulisemea japo aligusa kwa mbali.

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA