MAREKANI: WAZIRI WA ULINZI CHUCK HAGEL AJIUZULU


Barack obama amekubali Jumatatu Novemba 24 ombi la kujiuzulu kwa waziri wake wa ulinzi, Chuk Hagel.
Barack obama amekubali Jumatatu Novemba 24 ombi la kujiuzulu kwa waziri wake wa ulinzi, Chuk Hagel.
Na RFI
Waziri wa ulinzi wa Marekani Chuck Hagel, amewasilisha barua yake ya kujiuzulu Jumatatu Novemba kwenye Ikulu ya Washington. Kujiuzulu huko kumetangazwa na Chuck Hagel wakati wa mkutano na vyombo vya habari, mkutano ambao umehudhuriwa na barack Obama.
Kulingana na kauli ya Barack Obama, Chuk Hagel ndiye ametaka mwenyewe kutamatisha muhula wake kwenye wadhifa aliyokua akishikilia. Kati ya wawili hao hakuna aliyetoa maelezo zaidi kuhusu uamzi huo wa kujiuzulu. Lakini kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Marekani, waziri wa ulinzi alikua alipewa shinikizo
Gazeti la New York Times limebaini kwamba kujiuzulu kwa Chuk Hagel kunahusiana na hali ya kutoelewana iliyojitokeza katika vita vinavyoendeshwa na Marekani dhidi ya kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislam nchini Iraq na Syria.
Inasadikiwa kuwa Ikulu ya washington huenda ilikua ikitathmini mkakati wake dhidi ya wanajihadi na ilikua inahitaji mkakati huo uanze kutekelezwa na waziri mpya wa ulinzi. Chuck Hagel awali alikuwa na wajibu wa kusimamia uondoaji wa majeshi kutoka Iraq na Afghanistan, wala si kusimamia operesheni ya kijeshi.
Washirika wa karibu wa Barack Obama wamekanusha hoja ya kujiuzulu kutokana na kushinikizwa. " Hakuna tofauti ya maoni ambayo imesababisha Chuk hagel anachukua umazi huo wa kujiuzulu", maafisa wa Ikulu ya Washington wamesema. Maafisa hao wamebaini kwamba mazungumzo ya kujiuzulu kwa Chuk Hagel yalianza wiki mbili zilizopita.
Waziri wa Ulinzi ataendelea kushikilia wadhifa huo hadi atakapopatikana mrithi wake. Majina kadhaa tayari yameanza kutajwa, ikiwa ni pamoja na Michèle Fournoy, aliyekuwa naibu waziri wa ulinzi.

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA