PICHA: WAZIRI MAGUFULI APOKEA RASMI KIVUKO KIPYA KIKUBWA CHA MV DAR ES SALAAM


Leo Waziri wa Ujenzi Dk.Magufuli amekipokea rasmi kivuko cha MV DAR ES SALAAM kama utakvyokiona katika picha mbalimbali. Mbali na Dk.Magufuli wengine waliohudhuria mapokezi hayo ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Saidi Meck Sadiki Saidi, RAS wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Balozi H.Mlango (Katibu Mkuu Mstaafu - Ujenzi) ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya TEMESA, Mkurugenzi Mtendaji wa TEMESA, Kaimu Mkurugenzi wa Bandari Mhandisi Matei, Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam

Itakumbukwa waziri Magufuli amekuwa akiahidi kufanya jitihada za kupunguza msongamano katika Jiji la Dar es Salaam ikiwa ni pamoja na kununua kivuko kitakachofanya safari zake katika mwambao wa bahari ya Hindi mpaka Bagamoyo.

Kivuko hiki mkombozi wa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam kimejengwa na kampuni kutoka Denmark kwa gharama ya shilingi (Tanzania) bilioni 7.9.

Sifa kubwa ya kivuko cha MV DAR ES SALAAM:

1. Kina uwezo wa kubeba abiria kati ya 306 waliokaa hadi 400,

2. Kina spidi (speed) kubwa kuliko vivuko vyote Tanzania na hata Afrika ya Mashariki

3. Kina ghorofa mbili (Two Floors)

4. Kwa ndani kina makochi mazuri kabisa ya kisasa ikiwa pmoja na life jacket

5.Kina tekinorojia ya kisasa kabisa ya Nivigation.

Picha za matukio mbalimbali pindi Dk.Magufuli akikipokea kivuko:











Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA