NABII: KUELEKEA UCHAGUZI MKUU 2015 ITAKUWA NI BALAA

Stori: Chande Abdallah na Deogratius Mongela
NABII wa Kanisa la The Revelation lililopo Buza Kipera jijini Dar, Yaspi Bendera amesema uchaguzi mkuu ujao utakuwa balaa kubwa kufuatia maono anayoyaona wakati akishiriki ibada katika nyakati mbalimbali, Risasi Jumatano linakupa mkanda kamili.
Nabii wa Kanisa la The Revelation lililopo Buza Kipera jijini Dar, Yaspi Bendera.
Akizungumza wakati wa ibada kanisani kwake na baadaye na waandishi wetu Novemba 16 mwaka huu, Nabii Yaspi alisema kuna mgongano mkubwa miongoni mwa watu wanaotajwa kugombea urais, ili kumrithi rais Jakaya Kikwete ambaye alimwelezea kama kiongozi anayemuona kiroho kila mara.
“Nilimuona katika maono yangu kama mtu aliye kwenye majaribu makubwa kiroho, nikaandaa maombi hapa kanisani na tukamuombea kwa muda wa nusu saa na tunashukuru Mungu hali yake inaendelea vizuri baada ya kufanyiwa upasuaji wa tezi dume nchini Marekani. Bado namuona akiwa na maumivu kuanzia sehemu za kiuno, uti wa mgongo na shingoni mwake.
Mhe. Edward Lowasa.
“Hivi sasa ninapomuombea atasikia moto unawaka na kupita kwenye sehemu hizo na kuwa mzima kabisa. Tunamuombea baraka na uzima rais ili aweze kukabidhi madaraka vizuri kwa rais ajae,”alisema Nabii huyo na kuongeza kuwa alilazimika kumuombea rais ili asipatwe na madhara kwani kama hali hiyo ingetokea, kungekuwa na vurugu kubwa kuelekea wakati wa Uchaguzi mkuu.
Waandishi wetu waliokuwa eneo la tukio walimshuhudia Nabii Yaspi akiwa ameshika picha ya Rais na waumini wake wakizama katika maombi kwa ajili ya Rais Kikwete huku na walipomaliza alisema tatizo lake limemalizika.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda.
Kana kwamba haitoshi, Nabii huyo alisema baadhi ya wagombea urais wanapita kwa waganga wa kienyeji lakini akasema hawatafanikiwa kwa kuwa yeye anaomba Rais ajaye atoke kwa Mungu kwa kuwa yeye atakuwa nyuma ya mgombea huyo bila kujali chama anachotoka.
Nje ya ukumbi wa kanisa, Nabii huyo alizungumza na waandishi wetu ambao walimuuliza kuhusu jinsi anavyoona kuelekea uchaguzi mkuu wa mwakani.Vipi kuhusu utafiti wa Twaweza
Mwenyekiti wa CUF Prof. Ibrahim Lipumba.
Kuhusu utafiti uliotolewa hivi karibuni kuhusiana na uchaguzi mkuu kama ulivyowasilishwa na taasisi ya Twaweza, ambao umewagawa wananchi, Nabii huyo alisema anaunga mkono kwani umefanywa kwa usahihi kwa vile ndivyo hata yeye anavyoona.
“Utafiti umefanywa vizuri na nadhani kila kitu kipo kama kilivyoainishwa, lakini kama walivyosema wenyewe kwenye ripoti yao, upepo unaweza kubadilika wakati wowote maana miujiza ya Mungu huja bila kutarajiwa,” alisema.Nani atashinda Urais?
Wazari wa mambo ya nje Benard Membe.
“Hivi unauliza swali kama hilo kweli wakati huu? Ripoti iliyotolewa imemaliza kila kitu na majibu yako wazi kabisa,” alisema nabii huyo bila kutoa ufafanuzi zaidi.



Utafiti uliotolewa na taasisi hiyo ya Twaweza uliotolewa hivi karibuni, ulisema kuwa endapo Uchaguzi mkuu wan chi ungefanyika hivi sasa, Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa angeibuka mshindi, huku akifuatiwa kwa karibu na Waziri Mkuu wa sasa, Mizengo Pinda na Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Wilbroad Slaa akiibuka katika nafasi ya tatu.
Chanzo:GP

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA