BIRTHDAY PATI YA BABY MADAHA,YATAWALIWA NA UCHAFU 85%


Stori: Issa Mnally
SHEREHE ya siku ya kuzaliwa ya msanii wa muziki na filamu, Baby Joseph Madaha ‘Baby Madaha’ iliyofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita Kijitonyama jijini Dar es Salaam, ilitawaliwa na vitendo vichafu mwanzo mwisho.
Baby Joseph Madaha ‘Baby Madaha’akiogeshwa pombe na mashosti zake.
Hafla hiyo iliyohudhuriwa na watu wachache wakiwemo baadhi ya wasanii, ilifanyika katika Grosari moja iliyopo Kijitonyama.Miongoni mwa mastaa waliohudhuria alikuwa ni mcheza soka wa zamani wa timu ya Yanga ya jijini Dar, Samson  Mwamanda.
Sherehe hiyo iliyoanza mishale ya saa 6.00 usiku ilitawaliwa na vituko kibao vilivyowaacha midomo wazi baadhi ya wahudhuriaji.Moja ya vituko hivyo ni pale Baby Madaha aliyekuwa amekolea kwa kilevi alipoamua kupigana denda laivu na msanii Isabela Mpanda ambaye naye alikuwa kachangamka ile mbaya.
Baby Madaha akifurahia bethidei na shosti yake Isabela.
Isabela alikuwa kituko zaidi kufuatia kuvaa kinguo kifupi cha pinki kilichoacha sehemu kubwa ya mwili wake, hasa kuanzia mapajani kuwa wazi.
Msanii huyo pamoja na kujitupa huku na huko kilevi na kucheza muziki kwa kukata nyonga kinoma, alikuwa akiinua nguo yake juu na kuonesha kufuli lake ‘white’ na kujishika sehemu za nyuma jambo lililomfanya mmoja wa wahudhuriaji kusema:
Baby Joseph Madaha ‘Baby Madaha’akiwa amelowa pombe.



“Jamani pombe ni noma, mnaona mambo ya aibu anayoyafanya Isabela?”
Kituko kingine ni pale mastaa hao waliokuwa bwii kwa kilevi akiwemo Mwamanda, walipoamua kummwagia pombe kichwani na kwenye nguo zake Baby Madaha baada ya kumuimbia wimbo wa ‘Happy birth day to you…

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA