Kwa wale tusio na maslahi nao na wasiotuhusu, mara nyingi hatupendi kuwasifia wasikie kwa masikio yao. Tunapolazimika kufanya hivyo, mara nyingi ni ama kwa hofu ya ‘nitaonekanaje’ kwa maana ya kulinda kutokuonekana muungwana au kwa kujua kabisa kufanya hivyo hakutuathiri kwa vyovyote.
Ndio maana hutashangaa kuona hotuba za hadharani kuwaaga, kuwaenzi au kuwatambua watu fulani hujaa sifa. Sababu? Tunafanya hivyo kwa sababu kufanya kinyume hadharani ni hasara kwetu. Hatupendi kuonekana watu wa ajabu mbele za watu hata kama ndani kabisa ya nafsi tunaweza kuwa tunasema kinyume na tunachotaka watu wasikie. Nia ni ile ile, ‘Nionekane mtu mwenye hekima,’ maana yake napambana kujiweka kwenye nafasi ya juu.
Sasa unaweza kuelewa kwa nini kumsifu marehemu asiyesikia ni rahisi na kila mmoja wetu anaweza kufanya hivyo.
- Kwanza sifa kwa marehemu hazitutushi sisi tulio hai kwa sababu tunajua hana uwezo wa kujisikia vizuri hali ambayo wengi hatuipendi.
- Pili hatumkosoi kwa sababu tunajua hana uwezo wa kujisikia vibaya hali ambayo mara nyingi tunatamani itokee kama tulivyoona.
- Tatu, tunaogopa kushusha hadhi zetu kwa kumsemea vibaya marehemu hata kama tunajua alikuwa jambazi lililosumbua mtaani. Hofu ya kuonekana watu wa ajabu ndiyo ile nia tuliyokwisha izungumza ya kuhakikisha heshima zetu zinabaki juu.
Makala nzima ipo kwenye blogu ya Christian Bwaya - Jielewe:
Kwa nini ni rahisi kumsifia mtu akifa kuliko akiwa hai?
Comments
Post a Comment