NACTE INTER COLLEGE TANZANIA- DAR ES SALAAM BONANZA- JUMAMOSI HII 22/11/20149 (DIT)

PRESS  RELEASE
(Taarifa kwa Vyombo vya Habari)
Ndugu,  Waandishi wa Habari,
Siku ya jumamosi tarehe 22/11/2014 itakuwa ni siku ya Ufunguzi wa Michezo ya NACTE INTER COLLEGE TANZANIA, utakaofanyika kwenye viwanja vya Chuo cha Dar es salaam Institute of Teckinology (DIT) kuanzia saa mbili (2:00) asubuhi  mpaka saa kumi na mbili (12:00) jioni.
 itafanyika kila mwaka kwa kushirikisha vyuo mbali mbali  vya elimu ya kati  hapa nchini Tanzania na vilivyopata usajili wa kudumu wa NACTE ambapo Kanda mbali mbali za Tanzania kupitia vyuo vyao vitashindana katika michezo mbali mbali kwa wavulana na wasichana
Kampuni ya Miss Demokrasia Tanzania & Entertainment C.o Ltd,yenye makao makuu yake Mwenge  jijini Dar es Salaam kwa kushirikiana na wadau mbali mbali ndiyo itakayokuwa ikisimamia taratibu zote za michezo hiyo wakati wote wa mashindano.
Kwa upande wa mkoa wa dare s salaam vyuo vilivyopo katika orodha ni 105 hivyo kulingana na bajeti kuwa kubwa, kama imeweka utaratibu wa kushiriki wenye michuano hiyo ya NACTE ambapo ni vyuo 32 tu vitakavyokuwa vikishiriki baada ya kufanya mchujo wa awali kwa njia ya Bonanza na Timu mbili za juu kila BONANZA ndizo zitakazokuwa zikiingia katika idadi ya vyuo 32 vya NACTE ITER COLLEGE DAR ES SALAAM.
Siku ya jumamosi itakuwa ni sehemu ya kwanza( Season one) ambapo vyuo vilivyotaarifiwa kuhusika katika kuwania nafasi hizo mbili za juu ni pamoja na Wenyeji D.I.T, majirani zao C.B.E na wakongwe wa Michezo Chuo cha Usimamizi wa Fedha(IFM).
Vyuo vingine ni Dar es salaam City College(DACICO) na majirani zao chuo cha Mlimani Profesional, na Royal, na Timu Mwalikwa katika Season hiyo ni Timu ya 100.5 TIMES FM Radio, kwa kuwa katiba ya michuano hiyo inaruhusu kuhusisha timu mbili waalikwa ambao watatokana na vyombo vya habari ama chombo cha habari, hivyo 100.5 Times Fm, wakiwa pia ni kati ya wadhamini wakuu wa matangazo ya radio,  wamepata fulsa ya kushiriki hatua hii ya kwanza (Season one).
Michezo itakayohusishwa hiyo siku ya ufunguzi ni pamoja na Mpira wa Miguu, Netball, Basketball, na Voleyball na washindi wa kwanza watazawadiwa Kombe wakati washindi wa pili watapata Mpira Mmoja kutoka kwa Wadhamini Wakuu Kampuni ya Simu za Mkononi VODACOM .
Ukiachilia mbali michezo hiyo, michezo mingine itakayokuwa ikifanyika kati ya wanafunzi na wanafunzi ni DEBATE, Marathon, Modoling, Mashindano ya Vipaji  kwa viongozi wanaosimamia serikali za wanafunzi kwa nafasi za Rais na Makamu, Waziri Mkuu, Mawaziri wa Michezo,Fedha,  na Spika , watakaokuwa wakichuana katika kujielezea, kujibu maswali, na kuelezea Mada katika nafasi zao na changamoto wanazokabiliana nazo na washindi watakuwa wakipata tuzo mbali mbali kulingana na ushindi wa kila mmoja.
Mgeni Rasmi  katika Bonanza hilo ni Katibu mtendaji wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) na mgeni mwalikwa atakayekabidhi zawadi kwa washindi ni mkurugenzi mtendaji wa 100.5 -TIMES RADIO, Bw. Leule Nyaulawa.
Aidha nichukue fulsa hii kuwaomba ndugu zetu wandishi kuhamasisha Makampuni na wadau kujitokeza kudhamini michuano hii ambayo malengo yake ni kuendeleza vipaji na kuibua vijana watakaokuwa viongozi, pamoja na kuwajengea mazingira ya kushiriki mara kwa mara katika michezo kwani Micheo uleta udugu, Upendano, mshikamano, amani, Afya na pia kijana anayeshiriki mazoezi upata muda wa kutumia akili kutafakali mambo ya Maendelezo zaidi.
  Imetolewa na -Katibu Mkuu Miss Demokrasia Tanzania- HALIMA BAKARI

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA