JUMBA LA KIHISTORIA LA MJI MKONGWE LAPOROMOKA


Jumba moja kongwe liliopo eneo la Mji Mkongwe limeporomoka jana.

Jumba hilo lipo Jaws Corner kama unaendea Kanisa la Minara Miwili, kwenye kona ambapo nje huwa panauzwa vinyago. 

Nyumba hiyo zamani aliishi aliyekuwa Mwenyekiti wa mwanzo wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar, Mr Zubeir. 

Imeelezwa kuwa hakuna aliyeumia kutokana na kuanguka kwa jumba hilo kwa kuwa lilihamwa muda mrefu, hata hivyo inaelezwa kwamba kuna watu wawili walipita muda mfupi ndipo lilipoanguka jumba hilo bado haijafahamika kwamba watu hao walisalimika au wamefukiwa na kifusi cha jumba hilo. Vikosi vya ulinzi vilifika na kuanza kazi. Allah awasalim salama. 




Vijana wa Mji Mkongwe wakipiga picha na kutizama baadhi ya athari zilizotokea katika sehemu ya jumba hilo lililoporomoka liliopo Mji Mkongwe ambao ni Urithi wa Kimataifa



Sehemu la jumba lililoporomoka eneo la Mji Mkongwe, Jumba hilo limeporomoka jana

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA