Madai Wema avunja ndoa! ni ya Esma mdogo wake Diamond
Waandishi wetu HALI si shwari kwenye familia ya Kampuni ya Endless Fame Productions kufuatia madai mazito yanayomgusa mkurugenzi wake, Wema Isaac Sepetu akihusishwa na kuvunjika kwa ndoa ya mdogo wa mkali wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ almaarufu kwa jina la Esma Platnumz aliyeolewa na Hamad Manungwa ‘Petit Man’. MAI NDANI Katika sakata hilo, mtangazaji maarufu Bongo, Maimartha Jesse ‘Mai’, Esma na Mtangazaji Nasra Rajesh ‘Lady Naa’ wanadaiwa kuunda kundi lenye lengo la kuwasuta wezi wa waume za watu (Wema aliwekwa kwenye tageti) lililopewa jina la Al-Shabaab. Wakati mpango huo ukiendelea, Mai anadaiwa alielezea mkasa wa kuvunjika kwa ndoa ya Esma na Petit Man kwenye Instagram huku akimtaja Wema kuhusika kwa mafumbo, jambo lililomfanya staa huyo wa filamu (Wema) aogelee matusi ya kutosha. MADAI YA WEMA KUHUSIKA Madai kamili yanamhusisha Wema na uvunjifu wa ndoa hiyo akituhumiwa ‘kuchepuka’ na Petit Man kwa muda mrefu sasa huku mwenyewe akikanusha vikali. US...