Lowassa arudisha fomu za kuwania urais Chadema


LOWASA (2)
Makamu Mwenyekiti wa Chadema, Profesa  Abdallah Safari (kushoto)  akipokea fomu kutoka kwa Waziri Mkuu wa Zamani,  Edward Lowassa.
11826015_385630801629524_1277594260338425273_n
Ester Bulaya (wa kwanza kushoto waliovaa fulana) akiwa ukumbini kumshuhudia Edward Lowassa akirudisha fomu ya kugombea urais ndani ya chama.
LOWASA (4)LOWASA (5)LOWASA (6)LOWASA (7)LOWASA (8)
Wanachama wa Chadema wakimkaribisha Edward Lowassa kwa mabango wakati anarudisha fomu ya kugombea urais ndani ya chama.
LOWASA (10)
LOWASA (13)
Edward Lowassa akiwasili Makao Makuu kurudisha fomu za kuomba kugombea urais ndani ya chama, kushoto kwake ni Alfred Lwakatare, mkuu wa usalama wa chama.
LOWASA (11)LOWASA (12)Baadhi ya wageni waliohudhuria katika tukio la Edward Lowassa la kurudisha fomu ya kugombea urais.

HATIMAYE Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa leo amerejesha fomu ya kuomba uteuzi kuomba urais kupitia tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). Anaandika Sarafina Lidwino … (endelea).
Aidha, katika urejeshaji wa fomu Lowassa amepata udhamini kutoka mikoa 32 ambao amedhaminiwa na wanachama zaidi ya milioni 1.6
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Organaizesheni na Uchaguzi, Benson Kigaila amesema, wadhamini hao wamepatikana kutoka katika Kanda 10 na Mikoa 32 kwa nchi nzima.
“Sasa safari ya matumaini kupitia CCM imeishia njiani,safari ya uhakika kupitia Chadema imefika na kipindi hiki lazima kieleweke na tunaenda kuiondoa CCM madarakani asubuhi kweupe”,amesema Kigaila.
Ameongeza kuwa wanachama kutoka mikoa yote walikuwa wakitamani Lowassa apitie mikoa yote ili kumdhamini kutokana na muda mchache wameamua kumdhamini kupitia njia ya simu.
Kigaila ambae pia ni Mkurugenzi wa Kanda wa Mambo ya Uchaguzi wa chama hicho amesema wanachama wasijali chochote kwa kuwa baada ya mkutano mkuu kumpitisha mgombea ambao unatarajia kufanyika Agosti nne atachanja mbuga kuzunguka mikoa yote.
Nae Profesa Abdallah Safari ambae ni Makamu Mwenyekiti wa Chama Bara amesema amemshukuru Lowassa kwa kurejesha fomu hiyo kwa kuwa baadhi ya watu walidhani angeingia mitini kwa hiyo sasa tunajiandaa kwenda kuchukua dola.
Nae Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Salum Mwalimu amesema chama tawala hawawezi kuwasambaratisha chadema na kuja kwa Lowassa ni mpango wa mungu na nyama zote walizopanga hazitafanikiwa.

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA