Sheria ya mitandao itaanza kufanya kazi mnamo tarehe 01/09/2015, Jiepushe na haya



Elimu ndogo ninataka kushiriki nanyi ndugu zangu kupitia semina nikiwa kama mualikwa na mamlaka ya mawasiliano Tanzania ( TCRA ) mnamo tarehe 06 na 07/08/2015:
NOTE: Sheria ya mitandao itaanza kufanya kazi mnamo tarehe 01/09/2015 kwa maana hiyo basi hukumu za vifungo vinavyoambatana na faini za pesa nyingi zitafanyika kupitia vyombo vya sheria kwa kufuata utaratibu ( Polisi na Mahakama )
Vitu vya kujiepusha:
1. Kusambaza ujumbe wa uchochezi ama ushawishi wa kisiasa unaoweza kuleta athari kwa jamii yetu kupitia mitandao
2. Kusambaza au kutunga ujumbe unaoleta uchochezi wa kidini unaoweza kupelekea kuvuruga amani na maelewano kwa jamii kupitia mitandao
3. Kusambaza picha ama video za utupu ama zilizokosa maadilk kwa jamii kupitia mitandao mbalimbali ( Watsapp,Facebook,Youtube,Instagram n.k )
4. Kusambaza picha ama video za uchochezi wa kidini ama kisiasa kupitia makundi mbalimbali ama mitandao ya kijamii
5. Kushiriki kusambaza chochote kati ya vilivyotajwa hapo juu ��������( kutuma kama ulivyopokea ) itakughalimu
6. Wizi kupitia mitandao mbalimbali na mitandao ya simu utakughalimu
7. Kumpatia mtu line yako ya simu na kutumika kufanyia wizi ama utapeli itakughalimu
8. Kushiriki kumchafua mtu,taasisi,kikundi cha watu kwa namna yoyote kupitia mitandao pia itakughalimu 
9. Kupoteza simu bila kutoa taarifa na kufunga mawasiliano hayo yanaweza kupelekea kutumika kufanya uhalifu na ukaangukia hatarini 
10. Kutumia mtandao kwa utapeli kupitia brand ama jina la mtu itakughalimu 
Hukumu: Ni kifungo cha miaka kadhaa gerezani ama faini ya fedha isiyopungua milioni 5 kulingana na kosa lililofanyika
Kuepuka kuwamo kwenye adhabu hizi ni kuacha kushiriki kwa namna yoyote ile yote na mengine mengi yatakayotajwa zaidi kupitia elimu zaidi.
Vijana wengi ni waathirika wa hili suala kwa kuwa ndio wasiojua heshima ya mitandao
POLISI NA TCRA wakiwa na washirika wake wa Intelligency ( Intelijensia ) watakuwa mstari wa mbele kufanya ufuatiliaji wa kina kihusiana na hili zoezi endelevu kwa jamii yatu ya Tanzania
JIEPUSHE NA RUNGU HILI 01/09/2015 LINAANZA KUTEKELEZA KAZI

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA