NI WATU 10 PEKEE WANAOPINGA MUHULA WA 3 WA KAGAME

Maafisa nchini Rwanda wanasema kwamba baada ya mashauriano ya kitaifa ni watu kumi tu wanaompinga rais Kagame kuwania muhula wa tatu.
Gazeti la New Times lililo karibu na serikali linasema kati ya watu milioni mbili walioshauriwa kuhusu kufanyia katiba mageuzi ni watu kumi tu waliopinga fikra hiyo.
Katiba inasema rais anapaswa kuhudumu kwa mihula miwili pekee.
Wachambuzi wanasema raia wengi wa Rwanda huenda wameogopa kupinga pendekezo hilo.
Rais Kagame amehudumu madarakani tangu 1994.
(Taifa jirani la Burundi lilikumbwa na mgogoro mnamo mwezi Aprili baada ya rais Pierre Nkurunziza kuwania uhula wa tatu)
.CHANZO:BBC

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA