Ilani ya CCM yakamilika, Hakuna ahadi ya laptop, fedha
Ilani ya CCM 2015 |
Ndugu Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM akielekea kwenye ukumbi wa mkutano kwa ajili ya kuzungumza na waandishi wa habari, huku akiwa ameshikilia kitabu cha Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2015-2020 iliyopitishwa jana na Halmashauri Kuu ya CCM mjini Dodoma.
Ilani hiyo inayotarajiwa kuzinduliwa tarehe 25 Agosti ndiyo itakayotumika kwa kipindi cha miaka 5 ijayo iwapo Chama cha Mapinduzi CCM kitapewa ridhaa na wananchi kuongoza nchi kupitia mgombea wake wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli, katika uchaguzi mkuu ujao wa rais, Wabunge na Madiwani unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu kote nchini Tanzania.
Nape Nnauye amelaani na kuzikanusha taarifa zilizozagaa kwenye mitandao ya kijamii na baadhi ya magazeti kuandika kwamba Dk. John Pombe Magufuli alinukuliwa akisema atagawa kwa kila mwalimu kompyuta moja na kila kijiji shilingi milioni 50

"Jambo hili ni uzushi mkubwa kwani Ilani ya Uchaguzi ilikuwa haijakuwa tayari ndiyo imekamilika jana, Mambo hayo hakuna kwenye ilani ya Uchaguzi ya CCM ".Mkutano huo umefanyika katika Makao makuu ya CCM Ofisi ndogo Lumumba, Ijumaa ya Agosti 14, 2015.
“Hizi ni njama za kufanya CCM ionekane imeanza kampeni mapema wakati hatuwezi kufanya hivyo na tunajua sheria na taratibu za uchaguzi”.
Comments
Post a Comment