Kinachompa jeuri Mourinho dhidi ya Wenger kipo hapa
Kocha wa Chelsea Jose Mourinho ameingia tena kwenye headlines kwa kauli zake anazozitoa kuelekea mchezo wa Ngao ya Hisani, Chelsea itakutana na Arsenal leo August 2 saa 11 jioni kwenye uwanja wa Wembley wenye uwezo wa kuchukua mashabiki 90,000.Mourinho ambae anajulikana kwa kuwa na uwezo wa kucheza na akili ya kocha wa timu pinzani amerudi na kauli nyingine dhidi ya Wenger.
“Sifikirii kuhusu nini kilitokea nyuma, nafikiria kuhusu mechi mimi kushinda mechi sita, saba, nane au tisa bila kupoteza mechi hata moja haiweki utofauti wowote na sifikiri kama itasaidia chochote kwenye huu mchezo, mechi inayofuata kwangu haina mahusiano yoyote na mechi iliyopita “>>>Mourinho
Kocha wa Arsenal Arsene Wenger hajawahi kuifunga klabu ya Chelsea hata mara moja ikiwa chini ya Jose Mourinho, wachambuzi wa masuala ya soka wanatafsiri kauli zaMourinho kama ni njia ya kumdanganya kocha wa Arsenal Arsene Wenger ili ajiamini zaidi.
Mourinho amekuwa na rekodi nzuri dhidi ya kocha wa Arsenal kwani akiwa na kikosi cha Chelsea amewahi kucheza na Arsenal mechi 12 na kushinda mechi saba na kutoka suluhu mechi tano hivyo hiyo ni sababu inayoendelea kumtia jeuri
chanzo:millard ayo
Comments
Post a Comment