Shemeji wa ZARI aibula na kudai TIFFAH si mtoto wa Diamond!


Kazi ipo! Siku chache baada ya kuliona jua, mtoto wa kike ‘baby girl’ wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ aliyempata kupitia kwa mwandani wake, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, Latifah a.k.a Princess Tiffah anazidi kuwa gumzo.

TIFFAH SI WA DIAMOND?

Safari hii shemeji wa Zari ambaye ni rafiki mkubwa wa aliyekuwa mumewe wa ndoa aliyezaa naye watoto watatu wa kiume, Ivan Ssemwanga aitwaye King Lawrence ameibuka na kudai: “Tiffah si mtoto wa Diamond.”

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Uganda, King Lawrence, mwenye makazi yake nchini humo na Afrika Kusini ‘Sauz’ ameacha watu midomo wazi kwa kuendelea kusisitiza kuwa Tiffah ni damu ya Ivan.

GUMZO UGANDA

Vyombo hivyo vimeenda mbali zaidi kwa kudai kuwa Tiffah hafanani na Diamond bali Ivan, jambo lililoibua gumzo kubwa nchini humo.

Hata hivyo, vyombo hivyo vilidai kuwa kwa mujibu wa chanzo cha ndani ya familia ya Diamond, sura ya mtoto huyo ni Ivan mtupu kwani anafanana na wanaye watatu aliozaa na Zari.

KINARA NI KING LAWRENCE

Habari hizo zilieleza kwamba, King Lawrence ndiye amekuwa kinara wa kueneza habari hizo huku akimwita Ivan Baba Tiffah.

KIPIMO CHA DNA

Ilisemekana kwamba, King Lawrence amekuwa akisisitiza kuwa ili kumaliza ubishi mtoto huyo apelekwe Uganda kwa ajili ya Kipimo cha Vinasaba cha DNA (Deoxyribonucleic Acid) ambacho hupima chembe hai za binadamu zinazorithishwa kutoka kizazi hadi kizazi.

Chembe hizo za DNA hupatikana kutoka katika chembe hai nyeupe za damu. Mtu anayepimwa hutolewa sampuli ya damu au muda mwingine sampuli hutolewa ndani ya chembe za shavuni.

Kipimo hicho hufanyika katika maabara maalum na huchukua siku saba au zaidi kutoa majibu hivyo King Lawrence anadai ndicho kitasema ukweli.

HESABU ZINAKATAA?

Kwa mujibu wa vyombo hivyo vya habari, mara tu baada ya Zari kuripotiwa kuwa mjamzito huku Diamond akihusishwa, mumewe, Ivan aliibuka na kudai kuwa mkewe huyo wa zamani hawezi kuzaa na Diamond.

Ilisemekana kwamba, katika kipindi cha Novemba, mwaka jana ambapo ndipo Zari na Diamond walipokutana, hawakuwa na muda mrefu wa kujuana afya zao kiasi cha kutengeneza mimba hivyo wazo la kwamba Zari alikuwa tayari na mimba ya Ivan lilipewa nafasi kubwa.

“Unajua wanafanya calculations (hesabu) kutoka Novemba (mwaka jana) hadi Agosti (mwaka huu) wanadai kama ni kweli maana yake wawili hao hawakuchunguzana afya zao kwanza ndiyo maana hata kabla ya miezi tisa kamili tayari mtoto amepatikana.

“Hicho ndicho kigezo kingine dhaifu wanachokitumia watu wa Ivan bila kujua hata kama walikutana mara moja tu, mtoto angeweza kupatikana hata siku ya kwanza,” ilisomeka sehemu ya habari hizo zilizotawala mitandaoni nchini humo.

DIAMOND VIPI?

Jitihada za kumpata Diamond ambaye amekuwa akitamba na kumshukuru Mungu kwa kumjalia mtoto aliyemtafuta kwa muda mrefu ziligonga mwamba kufuatia simu yake ya kiganjani kutokuwa hewani kila ilipopigwa.

Chanzo: RISASI JUMAMOSI

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA