MSAJILI WA VYAMA AVIASA VYAMA VYA SIASA
MSAJILI wa Vyama Vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi amevitaka vyama vyote vya siasa kutekeleza wajibu wao kwa mujibu wa sheria , katiba na kanuni ili kuepusha migogoro.Aidha msajili huyo amevitaka vyama hivyo mfano mzuri wa kwa jamii kwa kudumisha amani na utulivu ndani ya vyama vya siasa.
Kauli hiyo imetolewa leo na Msajili huyo katika taarifa yake aliyoitoa kwa vyombo vya habari kufuatia kuwepo kwa wimbi kubwa la migogoro ndani ya vyama hivyo. "Endapo kwa bahati mbaya mgogoro ukiibuka, unatakiwa utatuliwe kwa utaratibu na namna ambayo itadumisha amani na utulivu ndani ya chama," alisema Jaji Mutungi.
Jaji Mutungi amewataka wanachama wa kawaida wa vyama vya siasa kupenda amani na utulivu ndani ya chama na kuepuka migogoro kwa kuheshimu na kufuata mfumo au taratibu za kuwasilisha malalamiko uliopo ndani ya chama au taasisi husika. Pia wawe wavumilivu mpaka watakapopata majibu ya malalamiko yao kutoka katika utaratibu huo uliowekwa na taasisi husika.
Aliongeza kuwa ofisi yake inajitahidi kuepusha na kutatua migogoro ndani ya vyama kwa kuchukua hatua zifuatazo, ambazo ni kuvihimiza vyama vya siasa kuheshimu sheria,kuzingatia misingi ya demokrasia na utawala bora,katiba na kanuni zake, kusuluhisha mgogoro unapoibuka, "Na hivi sasa tumewasilisha Serikalini mapendekezo ya marekebisho ya sheria yatakayosaidia kuepusha migogoro ndani ya vyama," alisisitiza.
Ameiomba jamii ikemee tabia ya migogoro isiyo na tija ,inapoona vyama vya siasa havitekelezi wajibu wake, badala yake vinajikita katika migogoro ndani ya ndani.
VICTOR SIMON
Comments
Post a Comment