TIKO ATAMANI KUOLEWA NA BABU MWARABU


Deogratius Mongela  
MSANII wa filamu  Bongo, Tiko Hassan ametoa ya moyoni na kusema kuwa kwa sasa yupo tayari kuolewa na babu Mwarabu ilimradi akitimiza mashariti yake.
Msanii wa filamu  Bongo, Tiko Hassan.
Akizungumza na Uwazi, Tiko alisema kwa sasa kama atatokea babu wa kumtolea posa, yupo tayari ila asiwe raia wa hapa bali awe Mwarabu maana vijana hasa wa Bongo sio waoaji ni wachezeaji.
“Kila mwanamke anatamani kuolewa, kama hujaolewa unaonekana kama muhuni na hata wazazi wako hawakupi heshima. Lakini kwangu mimi naona mababu wana raha yake bwana, kwanza wanaweza kutunza na kujali. Natamani sana niolewe na babu tena Mwarabu na haijalishi hata nikiwekwa mke wa tatu sawa tu,” alisema Tiko.

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA