"PROFESA WANGU KITILA MKUMBO HAPA SIJAKUELEWA VEMA

Mdahalo kwa wanaotajwa urais una maana gani?
Nina maswali mengine;
- Je, hatuoni kuwa kwa wanaojitaja urais au kutangaza nia wanapoandaliwa mdahalo ni sawa na kujifanyia kampeni za wazi kabla ya kipenga kupulizwa?
- Je, kama wanaojitaja au kutangaza nia si wagombea binafsi, bali wa vyama, hatuoni kuwa ni ajabu kuwa watashiriki mdahalo bila ya ilani za uchaguzi za vyama? Ina maana wata-debate juu ya namna watakavyotekeleza ' ilani za kusadikika'?!
Maswali ninayo mengi kwa Profesa Mkumbo ambaye ni Mkurugenzi wa Jumuiya ya Wanataaluma, Udasa. Waandaaji wa mdahalo.
Hili la mdahalo ni jambo jema kabisa, wasiwasi wangu tusije tukapoteza maana ya mdahalo. Kwamba kusanyiko la watangaza nia laweza kuwa ni usaili wa wazi tu wa watangaza nia badala ya kuita mdahalo.
Na kama lengo ni kuwafanya watangaza nia wafahamike na wapiga kura, tukubali , kuwa kama mtangaza nia ya kugombea urais, ikiwa imebaki miezi tisa kupiga kura hafahamiki kwa watanzania, basi, huyo hatufai kuwa Rais Wetu...
Maggid,
Dar es Salaam

chanzo:mjegwablog

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA