SITTI MTEMVU ATEMBELEA KITUO CHA WENYE ULEMAVU WA NGOZI HOSPITALI YA MKOA ILALA

Mbunge wa Jimbo la Ilala  Mhe Mussa Azzan Zungu akiongea na Waandishi wa Habari ( pichani hawapo)  mara baada ya kupokea  vifaa mbalimbali  vya kuhifadhia taka na Sabuni.
Mwenyekiti wa Sitti Tanzania Faundation, Sitti Mtemvu (wa tatu kulia) akimkabidhi vifaa vya kuhifadhia taka Mbunge wa Jimbo la Ilala  Mhe.  Mussa Azzan Zungu (kushoto), kwa ajili ya Hospitali ya Mkoa wa Ilala Dar es Salam.  kuanzia kushoto  nyuma ya mbunge ni Diwani wa kata ya Kinyerezi kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Leah Mgitu katikati ni mama mzazi wa Sitti Mariam Mtemvu, wa kwanza kulia ni Diwani wa Kata ya Ilala kupitia Chama cha Mapinduzi  Edson Fungo na anaefuatia ni  Daktari Kiongozi wa Hospitali ya Mkoa Ilala
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Under The  Sun Tanzania  Bi. Vicky Ntetema (kulia) , akifafanua jambo wakati Mwenyekiti huyo alipotembelea kituo hicho
Afisa utetezi  Bw. Kondo Seif (wa kwanza kushoto)  akitolea maelezo ya ukosefu wa rangi asili mwilini ambayo huathiri ngozi, macho na nywele na kukosekana kwa  melani mwilini, akisema miongoni mwa athari zake ni wepesi wa kuungua na jua unapotembea juani na ufanyapo kazi juani.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Under The  Sun Tanzania  Vicky Ntetema (kulia) akimuonyesha Mwenyekiti wa Sitti Tanzania Foundation,  Sitti Mtemvu (kushoto)  Picha ya mtoto  alie tekwa akiwa mgongoni mwa mama yake. Wa pili  kushoto ni Mama mzazi  wa Sitti.


Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA