WAZIRI WA MAJI JUMANNE MAGHEMBE AMETOA SIKU 90, KWA MKANDARASI MEGHA ENGINEERING

unnamed (2)Waziri wa maji Jumanne Maghembe wa kwanza kulia akizungumza na wakandarasi wanaojenga bomba la maji la Mlandizi Kimara Januari 20, 2015 mkoani Pwani wakati alipotembelea tembelea miradi ya maji inayosimamiwa na Mamlaka ya Maji Safi na maji Taka (DAWASA),  kwalengo la kupata tathimini ya mradi huo ulipofikia sasa.unnamed (4)Waziri wa Maji Jumanne Maghembe wapili kulia akioneshwa mchoro wa mradi wa bomba la maji  mlandizi kimara linalopitia makongo juu na Mhandisi wa Mradi huo, Bw Severin Mkendala jinsi mabomba  mradi wa mlandizi kimara yalipopita .unnamed (10)Waziri wa maji Jumanne Mghembe wa pili kulia akiwa ameongozana na meneja mradi Pintu Dutta watatu kulia wakati akikagua maendeleo ya mradi wa kituo cha kusafisha maji cha ruvu juu .
unnamed (6)Mashine aina ya Catterpilar la kampuni ya Megha Enginearing Infastructure Limited, likiwa linasafisha eneo ambalo linatakiwa kulazwa mabomba ya yanayotoka Mlandizi Kimara kwenda Ruvu JUU.unnamed (7)Kushoto ni Meneja Mradi kutoka Kampuni ya Megha Engenearin Infastructure Limited Mural Mohan, akimweleza maendeleo ya mradi huo Waziri wa Maji Jumanne Maghembe,aliyekuwa katika ziara  ya kutembelea miradi  inayosimamiwa na Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka.unnamed (8)Waziri wa Maji Jumanne Maghembe akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukamilisha ziara hiyo. 
unnamed (5)Wafanyakazi wa kampuni ya WABAG Constraction wakiendela na ujenzi wa wa kituo cha kuasfisha maji cha ruvu juu .
…………………………………………………………………………………….
WAZIRI wa maji Jumanne Maghembe ametoa siku 90, kwa mkandarasi Megha Engineering Infrastructure Limitedi anaesambaza bomba la maji mradi wa Mlandizi Kimara kufanikisha mradi huo na kupeleka ripoti ya maradi,mamlka ya maji safi na maji taka (Dawasco), kwalengo la kupata tathimini ya mradi.
Alitoa agizo hilo Januari 20, 2015 mkoani Pwani wakati akikagua miradi minne ya Dawasco,yakusambaza maji Ruvu juu na Ruvu Chini kufikisha Jijini Dar es Salaam.
Alisema,mpaka sasa mkandarasi alitakiwa aweamelaza kilomita 20,lakini chakushangaza mkandarasi huyo amelaza kilomita 12,tu.
Maghembe alisema utendaji kazi wa mkandarasi huyo ni mbovu na nimewaagiza wabadilike na nitakuja kuwatembelea baada ya siku 90,na kama hakutakuwa na maendeleo itabidi tuwafukuze.
“tumempatia mkandarasio huyu kiasi cha dola za kimarikani 59,ambao nisawa na bilioni 96 za kitanzani fedha hizi watanzania watazilipa hivyo ni vema mkandarasi huyu afanye kazi iliyomleta,”alisema Maghembe
Kwaupande wa maradi wa Ruvu juu wa kusafisha maji Waziri Maghembe aliridhika na utendaji kazi wa mkandarasi anayejenga mradi huo na kumtaka amalizie kufunga pampu mpya ili mgao wa maji upungue Dar es Salaam.
Aidha alimwagiza Mkurugenzi Mkuu wa DAWASA Arcado Mutalemwa kuhakikisha pampu zilizokwama bandarini zinafika leo na kufungwa siku ya Alhamisi.

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA