MADAI YA KUBEBA UNGA:RAY C AJISALIMISHA POLISI

Stori Na Musa Mateja/Ijumaa Wikienda
BAADA ya kukiri kwa mdomo wake kutumia madawa ya kulevya ‘unga’ na baadaye ‘kustaafu’, madawa hayohayo yamemletea msanii Rehema Chalamila ‘Ray C’ ‘msala’ ambao umemfanya yeye mwenyewe, kwa hiyari yake ajisalimishe polisi.



Msanii wa Bongo Fleva, Rehema Chalamila ‘Ray C’ akiwa Hospitali ya Mwananyamala .

Hivi karibuni, Ray C alijikuta akiangua kilio ndani ya Kituo cha Polisi cha Kijitonyama ‘Mabatini’, Dar baada ya kuhusishwa na ishu ya uuzaji wa unga.

KAWE DARAJANI
Chanzo hicho kilinyetisha kwamba, siku ya tukio, wakati Ray C akitokea nyumbani kwake, alipofika maeneo ya Kawe Darajani aliona pikipiki ikimfukuzia na baadaye ikampita na ‘kumbloku’.
Ilisemekana kwamba baada ya kusimama, jamaa alishuka kwenye pikipiki kisha akamwambia aegeshe pembeni gari lake aina ya Toyota Carina TI.

Chanzo kilidai kwamba, Ray C alikataa kufanya hivyo kwa kuhisi aliyekuwa akimwamrisha ni jambazi.
“Ray C aliamua kuondoa gari kwa kulazimisha ambapo alimkwepa jamaa huyo kisha kukanyaga mafuta ambapo gari liliondoka kwa kasi,” alisema.

LUGALO
Ilisemekana kwamba baada ya kufika kwenye kituo cha daladala cha Lugalo, alisimama na jamaa huyo aliyekuwa akimfukuzia akaegesha pikipiki mbele yake na kumtaka Ray C ashuke ndani ya gari kwani alitaka kulipekua akimwambia kuwa alikuwa amebeba unga.
Ishu hiyo ilizidi kumtia Ray C wasiwasi na kumuuliza jamaa huyo ni nani ambapo alisema kuwa yeye ni askari.
Kwa kuwa hakuwa na sare, Ray C hakuamini jambo lililosababisha jamaa huyo kumuonesha kitambulisho kilichokuwa kimechakaa.

‘Ray C’akiingia kwenye gari lake aina ya 'Toyota Carina'.

MAELEWANO YASHINDIKANA
Baada ya kuona hivyo, Ray C alimwambia waongozane hadi Kituo cha Polisi cha Oysterbay lakini jamaa huyo alikataa na kumtaka waende Kawe jambo ambalo Ray C alishindwa kuafikiana nalo na kuondoa gari lake akimwambia waambatane hadi Kituo Kidogo cha Polisi cha Mwenge.

Jamaa huyo alionekana kutotaka kwenda hivyo Ray C aliondoa gari kwa kasi na kuelekea Mwenge ambako alikuwa akiomba msaada kwa matrafiki na alipoona wanachelewa aliondoa gari kumkimbia jamaa huyo.
Ilisemekana kwamba awali alitaka kukimbilia Kituo cha Polisi cha Mwenge lakini alipoona kuna msongamano alikimbia kwenda kujisalimisha Mabatini huku akiangua kilio.

BOFYA HAPA KUMSIKIA RAY C
Baada ya kushibishwa taarifa hiyo, Ijumaa Wikienda lilimtafuta Ray C ambaye alielezea mkasa mzima.
Alifunguka: “Ni kweli ulivyoambiwa tulitoka Lugalo na kuelekea Mwenge baada ya kufika kwenye makutano ya Mwenge niliwaona askari wawili na trafiki akiwa pembeni, nikawasimamisha na kuwaeleza.
“Askari mmoja alikubali kupanda kwenye gari langu nikaenda naye hadi Mabatini.

“Baada ya kufika Mabatini nilieleza kila kitu kwa mkuu wa kituo hivyo akaniambia nisiwe na wasiwasi.
“Bada ya hapo mkuu wa kituo aliita askari wa kike na wa kiume nikaongozana nao hadi katika gari langu na kupekua kila sehemu lakini wakasema hapakuwa na chochote kibovu, hivyo nikawa nalia tu na mkuu wa kituo akaniomba ninyamaze na kuniruhusu nikaondoka zangu kwenda Hospitali ya Mwananyamala kumeza dawa.

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA