MWANAMKE AKAMATWA KWA UNGA WA BIL.2 NYUMBANI KWA MBUNGE

Na Makongoro Oging’/Uwazi
MWANAMKE mmoja aliyetambuliwa kwa jina la Doreen John Mlemba, mwenyeji wa Same mkoani Kilimanjaro, mwishoni mwa mwaka uliopita alikamatwa kwa kuhusishwa na shehena ya madawa ya kulevya aina ya Heroin, yenye thamani ya shilingi bilioni 2.5.
Madawa hayo yalikutwa kwenye nyumba moja iliyopo eneo la Ununio, Tegeta jijini Dar es Salaam, ambayo ni mali ya Mbunge wa CCM (Jina linahifadhiwa) wa jimbo moja la mikoa ya Kanda ya Ziwa, Uwazi limefukunyua.
Taarifa toka vyanzo mbalimbali makini, zinasema majirani wa…
Mwanamke (Doreen John Mlemba) anayedaiwa kukamatwa na unga.
Na Makongoro Oging’/Uwazi
MWANAMKE mmoja aliyetambuliwa kwa jina la Doreen John Mlemba, mwenyeji wa Same mkoani Kilimanjaro, mwishoni mwa mwaka uliopita alikamatwa kwa kuhusishwa na shehena ya madawa ya kulevya aina ya Heroin, yenye thamani ya shilingi bilioni 2.5.
Madawa hayo yalikutwa kwenye nyumba moja iliyopo eneo la Ununio, Tegeta jijini Dar es Salaam, ambayo ni mali ya Mbunge wa CCM (Jina linahifadhiwa) wa jimbo moja la mikoa ya Kanda ya Ziwa, Uwazi limefukunyua.
Taarifa toka vyanzo mbalimbali makini, zinasema majirani wa nyumba hiyo walikuwa na mashaka na kinachofanyika ndani ya nyumba hiyo, kwani licha ya ukubwa na kukamilika kwa ujenzi wake, lakini haikuwa ikikaliwa na mtu na mara chache, watu walionekana wakiingia na kutoka bila kujulikana walichokuwa wakikifanya.
Kutokana na hali hiyo ya wasiwasi, wasamaria wema walitoa taarifa kwa Jeshi la Polisi ambalo liliifanyia kazi habari hiyo na kufika kwenye nyumba hiyo na kujaribu kugonga lakini bila mafanikio yoyote.
“Baada ya kugonga, ndipo polisi hao walipoamua kuvunja mlango na kufanya upekuzi katika sehemu zote ndani ya nyumba hiyo, ambapo walifanikiwa kulikuta sanduku ambalo baada ya kufunguliwa, zikagundulika kilo 35 za madawa ya kulevya aina ya Heroin,” kilisema chanzo chetu kilichoshuhudia zoezi hilo.
Kamanda wa Kikosi Cha Kupambana na Kudhibiti Madawa ya Kulevya nchini, SACP Godfrey Nzowa alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa baada ya kukamata shehena hiyo, vijana wake walijikuta katika wakati mgumu wa kumjua mmiliki wa nyumba hiyo.
Hii ni nyumba aliponaswa mwanamke huyo akiwa na unga.
Baada ya kutafuta nyaraka mbalimbali, hatimaye waligundua kuwa nyumba hiyo inamilikiwa na mbunge huyo wa zamani ambaye alitafutwa na kuhojiwa kwa saa kadhaa, ambapo alikiri kuimiliki, lakini akidai kwa muda huo, alikuwa ameipangisha kwa watu aliowataja, bila kujua shughuli iliyokuwa ikifanyika ndani yake.
Inadaiwa kuwa baada ya kupata ushirikiano huo kutoka kwa mbunge huyo, askari waliingia mtaani kuwasaka wapangaji hao, ambapo Septemba 15, mwaka jana, saa saba mchana, walifanikiwa kumkamata Doreen, akiwa shambani kwake, eneo la Ruaha Mbuyuni mkoani Iringa alikokuwa akivuna vitunguu, bamia na bilinganya.
“Tulifanya uchunguzi na tayari watu watano wameshakamatwa akiwemo Doreen, nyumba hiyo waliifanya kama ghala la kuhifadhia madawa na mtu mmoja bado tunaendelea kumsaka, baadhi ya waliokamatwa tulikuwa tukiwasaka kwa muda mrefu,” alisema Kamanda Nzowa.
Aliwashukuru wananchi kwa ushirikiano wao na kuwaomba waendelee hivyo na kwamba donge nono litatolewa kwa watakaofanya hivyo huku majina yao yakihifadhiwa.Gazeti hili lilimfikia Mbunge huyo mmiliki wa nyumba kwa njia ya simu, lakini alikataa kulizungumzia suala hilo, akidai liko chini ya polisi.



“Naomba suala hili umuulize Kamanda Nzowa, mimi siwezi kulizungumzia kwa vile lipo chini ya uchunguzi wao, pamoja na kwamba nawatambua hao wapangaji lakini siwezi kusema lolote,” alisema.

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA