VIONGOZI WA SIMBA WAPATA AJALI.

Gari la kiongozi wa simba matawi ya temeke lililopata ajali ya kugonga ngombe katika eneo la Mhoro barabara ya kilwa jana picha na Sultan Mkwera

Gari hilo lililogonga ng'ombe likiendeshwa na dereva Method Mathew ambaye alikuwa na wenzake ambao jumla ni watano ndani ya gari hilo Toyota aina ya Prado lenye namba za usajili T439 CFT.


Mwandishi habari aliekuwa huko Muhoro amesema gari hilo liligonga ng'ombe waliokuwa wanavuka barabara wakati dereva akijitahidi kufunga breki. Gari hilo liliserereka likawagonga ng'ombe kadha, ambapo wawili walikufa papo hapo huku wenginge wakijeruhiwa na kushindwa kutembea. 

Ajali hiyo ilitokea katika eneo la Kibiti, Lindi majira ya saa 11 jioni ya Jumapili wakati viongozi wa matawi ya Simba vilayani Temeke jijini Dar es Salaam wakirudi kutoka mkoani Mtwara kwenye pambano la Simba SC na Ndanda FC kwenye mchezo uliochezwa Jumamosi wa ligi kuu ya Vodacom.

Mchungaji wa mifugo alikimbia katika eneo lakini baadaye alijitokeza katika kituo cha polisi cha Muhoro na kujisalimisha mwenyewe. Alitambulika kwa jina moja tu la Lufunga. Anashikiliwa na polisi.



  • Habari kutoka: mzukakamili-mzuka.blogspot.com

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA