Posts

Showing posts from February, 2015

MAMA SALMA KIKWETE AKABIDHI MASHINE YA KUPIMIA SARATANI YA MATITI KWA AKINA MAMA HOSPITALI KUU YA JESHI LUGALO

Image
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA Mama Salma Kikwete akikabidhi mashine ya kupimia saratani ya matiti kwa akina mama kwa uongozi kwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi Luteni Jenerali Samuel Ndomba (kulia). Hafla ya makabidhiano hayo ilifanyika kwenye Hospitani Kuu ya Jeshi Lugalo kwenye Kitengo cha Uzazi na Mtoto kilichoko Mwenge tarehe 27.2.2015. Aliyesimama pembeni kwa Mama Salma ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Donan Mmbando na aliyesimama kulia kwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi ni Mkuu wa Hospitali Kuu ya Jeshi ya Lugal Brigedia Jenerali Josia Mwita Makere Baadhi ya viongozi wa Jeshi la Ulinzi na wananchi waalikwa wakisikiliza kwa makini hotuba ya mgeni Rasmi Mama Salma Kikwete wakati wa hafla ya kukabidhi mashine ya kupimia saratani ya matiti kwa akina mama. A Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA, Mama Salma Kikwete akitoa hotuba yake muda mfupi kabla ya kukabidhi mashine ya kupimia saratani ta matiti kwa ak...

NEW VIDEO: JUA CALI "KARIBU NAIROBI"

Image
Burudika hapa na video mpya ya Jua Cali ‘Karibu Nairobi’. Enjoy.

NDOA YA TEMBA YAPUMULIA MASHINE

Image
MWANDISHI WETU NDOA  ya msanii nyota wa muziki wa kizazi kipya nchini, Amani James ‘Temba’ inadaiwa kupumulia mashine kutokana na madai ya kuwepo kwa usaliti baina yao. Msanii nyota wa muziki wa kizazi kipya nchini, Amani James ‘Temba’ akiwa na mke wake siku ya ndoa yao. Habari kutoka kwa chanzo kilicho karibu na wanandoa hao wanaoishi wilayani Temeke, kinasema kumekuwa na mgogoro wa muda mrefu baina ya watu hao, kila mmoja akimtuhumu mwenzake kusaliti, jambo linaloonyesha wakati wowote ndoa yao inaweza kusambaratika. “Jamaa hayuko ‘peace’ kabisa na ndoa yake, yaani kila siku ni mgogoro, wife wake anamshutumu mshkaji kuwa msaliti kwa wanawake wengine na mke naye anatuhumiwa hivyohivyo ili mradi hakuna amani kabisa. Inaonekana kuna tatizo kubwa,” kilisema chanzo hicho kilichoomba hifadhi ya jina lake. Gazeti hili halikuweza kuwapata wanandoa hao kutokana na simu zao kutopatikana, lakini wakati linakwenda mitamboni, lilipata taarifa za kufikishwa mahakamani kwa Mhe...

CHEKECHA CHEKETUA - ALI KIBA UPO HAPA DOWNLOAD HAPA

Image

SOMA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI HAPA

Image
 m

WANABLOGU TANZANIA KUJUMIKA LEO KWENYE PARTY @SERENA HOTEL

Image
Mwenyekiti wa Tanzania Bloggers Network na mmiliki wa Blog ya The Habari.com, Joachim Mushi (katikati) akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari. Kutoka kushoto ni Mkala Fundikira, Afisa wa kampuni ya mawasiliano na matangazo ya AIM Shafiq Mpanja , Ofisa Uhusiano wa NMB bi. Doris Kilale na Khadija Kalili. Katika mkutano huo TBN imesema leo Jumamosi jioni  Bloggers  takriban 100 kutoka sehemu mbalimbali nchini watakutanika katika ukumbi wa hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam kwa ajili ya hafla ya mwaka mpya itayohudhuriwa pia na wadhamini na marafiki wa Bloggers. Ofisa Uhusiano wa NMB Doris Kilale akifafanua jambo wakati wa mkutano. Mmiliki wa Blog ya Bongoweekeend Khadija Kalili akizungumza wakati wa mkutano. Father Kidevu (kulia) akifafanua jambo wakati wa mkutano. Baadhi ya Bloggers na waandishi wa vyombo mbalimbali vya Habari wakifuatilia jambo wakati wa mkutano uliofanyika katika Ofisi za Idara ya Habari Maelezo Dar es Salaam. 

UZINDUZI WA KIVUKO CHA DAR ES SALAAM

Image

RAIS WA ZIMBABWE ATIMIZA MIAKA 91 LEO KUFANYIWA SHEREHE

Image
Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe. Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe,ametimiza  miaka 91 leo , katika sherehe yake ya kuzaliwa atachinja tembo wawili. Sherehe hizo zitafanyika kwenye mji wa Victoria Falls na zinaandaliwa na chama tawala ZANU-PF kinataka kukusanya dola za Kimarekani milioni 1 kwa ajili ya sherehe ya kesho. Wageni wapatao 20,000 wanatarajiwa kuhudhuria. Hata hivyo, mashirika ya kutetea ulinzi wa wanyama pori yamemkosoa Mugabe, wakisema haiwezekani akakemea uharamia wakati yeye mwenyewe anaamuru wanyamapori wachinjwe. Pamoja na hayo baadhi ya raia wa Zimbabwe wanakerwa na uamuzi wa rais wao kufanya sherehe kubwa kama hiyo, wakati wananchi wake wengi ni maskini.

KANISA LA MCHUNGAJI GWANJIMA LAPEWA NOTISI YA KUFUNGASHA VIRAGO KAWE

Image
Mch. Gwajima Kanisa la lisilo rasmi la mchungaji Mchungaji Josephat Gwajima lililokuwa likiendesha shughuli zake kinyume na taratibu katika viwanja vya Tanganyika Packers Kawe, wilaya ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam limeamriwa kuondoka mara moja na kuacha eneo hilo wazi kwa ajili ya maendeleo ya watu wa Kawe.  Kanisa hilo kwa muda mrefu lemekuwa likiendesha shughuli zake kinyume na taratibu na kusababisha usumbufu na kero kubwa za makelele kwa wakazi wa maeneo hayo.  Barua iliyosainiwa na Meneja wa Mkoa wa Kinondoni wa Shirika la Nyumba la Taifa imesisitiza kwamba pamoja na kutambuliwa umuhimu wa Kanisa hilo kuendesha shughuli zake, bado shirika hilo halitaweza kutoa ruhusa kwa kanisa hilo kuendelea kufanya mahubiri katika viwanja hivyo, kwani shirika hilo limeshaanza kutumia viwanja hivyo kwa maendeleo ya wananchi wa Kawe kwa ujenzi wa makazi ya watu. Bw Masika ametoa nositsi ya siku 30 tu kwa Mchungaji Gwajima kuwa ameshaacha viwanja hivyo wazi. T...

MASTAA 10 BONGO WANAOVAA NUSU UTUPU SIYO ISHU KWAO

Image
Ukifuatilia sana kwenye nchi za wenzetu kama vile Marekani na kwingineko, mastaa hawako makini na suala la uvaaji. Yaani si ajabu kuona staa mkubwa akikatiza mtaani akiwa amevaa nguo ya ndani na ukishangaa utaonekana mshamba. Jokate Mwegelo. Wanaovaa hivyo hawajakosa nguo za heshima za kuvaa bali ni ule ulimbukeni wa kutaka wawe gumzo na kuendelea kuwa maarufu.Kutokana na athari ya utandawazi, hapa Bongo wapo mastaa ambao nao wameiga kiasi cha kutoona aibu kuvaa nguo zinazoacha wazi maungo yao.Najua wapo wengi lakini leo nimeona nikupe kumi bora ya mastaa hao. Baby Joseph Madaha Huyu ni mwanamuziki na muigizaji. Wengi wanamfahamu kwa kupenda kuyaacha wazi matiti yake sambamba na kupenda kuvaa visketi na vigauni vinavyoacha wazi sehemu kubwa ya mapaja. Stejini ndiyo kabisa hadi kufuli lake kama siku hiyo amelivaa haoni aibu kulifanya lionekane kwa mashabiki wanaofuatilia shoo yake. Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’ Ni muigizaji aliyejaribu kuingia kwenye muziki lakini akashindwa. N...