Taarifa ya IFM Students Organisation kuhusu 'kumpigia debe' Lowasa



TAARIFA KWA UMMA

SERIKALI YA WANAFUNZI CHUO CHA USIMAMIZI WA FEDHA (IFM-SO) YAKANUSHA KUMPIGIA DEBE LOWASA.


Serikali ya wanafunzi wa chuo cha usimamizi wa fedha (IFMSO), kupitia msemaji wake mkuu ambaye ni Rais wa Serikali ya wanafunzi, ndugu Clinton Boniface inakanusha taarifa zilizotolewa na gazeti la NIPASHE
toleo namba 0578395 la tarehe 19/02/2015, lenye kichwa cha habari “WANAFUNZI WA IFM WAMTAKA LOWASA URAIS” na kwamba habari hizo hazijatolewa na uongozi wa IFMSO, wala hakuna mkutano wowote uliofanyika katika eneo la chuo cha usimamizi wa fedha kati ya waandishi wa habari na uongozi wa serikali ya wanafunzi na kutoa tamko hilo. Pia, kulingana na Katiba ya IFMSO kifungu namba 3, ibara ndogo ya 1, Katiba inakataza serikali ya wanafunzi (IFMSO) kushiriki katika mambo yoyote ya kidini au kisiasa, hivyo basi IFMSO inasikitishwa na taarifa hizo na inaomba radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza kutokana na taarifa hizo.

Imetolewa na;

…..........
Clinton Boniface
Rais wa Serikali ya Wanafunzi
IFM-SO
19/ 02/ 2015

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA