MAJIBU YA JAY DEE NA GARDNER KUACHANA YAPO HAPA

 
Gardner G Habash na Judith Wambura Mbibo ‘Lady Jay D’ siku ya harusi yao.
Ishu hiyo iliyopata nafasi kwenye vyombo mbalimbali vya habari, ilitokana na Jide kuwapa watu nafasi mashabiki wake kumuuliza maswali katika mtandao wa kijamii, ambapo asilimia kubwa walitaka kujua kama kweli ameachana na mume wake au la.
Magazeti Pendwa kutoka Global Publishers yakaamua kumtafuta Gardner ili aweke bayana juu ya suala la ndoa yao kutokana na mwanamuziki huyo kuweka wazi kwamba tayari ndoa yao ilikwishasambaratika.
“Alichokisema na ulichokisikia ndiyo ukweli wenyewe. Hakuna ndoa tena, tumekwishaachana na kila mmoja kuchukua kilicho chake. Ila kila kitu namwachia Mungu na wala sina kinyongo naye,” alisema Gardner.

...Wakiwa kwenye pozi.
Siku chache zilizopita mwanamuziki Jide alifunguka kwamba hakutaka tena kuendelea kuishi na mume wake kutokana na tabia mbaya alizokuwa nazo mwanamume huyo,  hali iliyomfanya kuishi pasipo kuwa na furaha katika kipindi kirefu cha ndoa yao.
Akifunguka zaidi, Jide alisema kwamba alichoshwa na tabia hizo ambazo alipobanwa zaidi ili aziweke wazi tabia hizo, alisema kwamba mwanamume huyo alikuwa na tabia ya kuwashikashika wanawake kila alipokuwa jukwaani akiimba. 
 
Alipenda kuwatongoza wanawake wengi tu ambapo  kuna siku alimkuta akimshikashika mapaja mwanamke ndani ya mghahawa wake, na alipomuuliza, alikiri kufanya hivyo na kuomba msamaha.
Wawili hao walifunga ndoa Mei 14, 2005, jijini Dar es Salaam ambapo mpaka wanaachana, hawakubahatika kupata mtoto.

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA