WATU WATU WAKAMATWA NA SMG, MAPANGA, VITAMBAA VYEUSI VITATU

WATU 3 wanaodhaniwa kuwa ni majambazi ambao walikuwa na silaha inayodaiwa kuwa ni SMG pamoja na mapanga huku wakiwa wamejifunga vitambaa vyeusi usoni walivamia kituo cha mafuta cha Jamuhuri Petrol Filling Station kilichopa katika eneo la mtaa wa Kalanje mjini Tunduru mkoani Ruvuma na kupora fedha taslimu shilingi milioni 7/= pamoja na simu moja ya mkononi yenye thamani ya shilingi laki tisa na elfu themanini kisha walikimbia na kutokomea kusikojulikana.

Akizungumza na waandishi wa habari jana ofisini kwake, Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Ruvuma, Mihayo Msikhela alisema kuwa tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa 3 na nusu usiku.

Amedai siku hiyo ya tukio watu hao waliwatisha kuwapiga risasi wafanyakazi wa kituo hicho huku wakidai fedha walizokuwa nazo na baadaye kufanikiwa kunyang’anya fedha hizo na simu (Samsung Galaxy). Imedaiwa kuwa waliwawekwa chini ya ulizi wafanyakazi wa kituo hicho akiwemo Nasri Salum (27) mwenye (mwenye aisli ya Kiarabu) aliyekuwa anakamilisha mahesabu ya mauzo ya siku hiyo.

Alifafanua zaidi kuwa awali majambazi hao walifika katika kituo hicho kama wateja wengine wakiwa na gari na baada ya kuhudumiwa walienda kulipa fedha dirishani ambapo ghafla walitoa bunduki na kufyatua risasi mbili hewani kisha kutoa mapanga.

Baada ya kuporwa, wafanyakazi walikimbilia Kituo Kikuu cha polisi kutoa taarifa ambapo askari polisi walikwenda kwenye eneo la tukio na baada ya uchunguzi waligundua maganda mawili ya lisasi yaliyotumika na walipoyafanyia uchunguzi ilibainika kuwa ni risasi ya bunduki aina ya SMG.


  • Taarifa ya Mpenda Mvula, Songea via blog

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA