ETIENNE KABILA ANAYETUHUMIWA KUMPINDUA RAIS JOSEPH KABILA AACHIWA HURU

Etienne Taratibu Kabila

Mahakama kuu ya Pretoria imemuachilia huru mwanasiasa wa upinzani, Etienne Kabila, ambaye anadai kuwa mtoto wa kwanza wa raias wa zamani wa jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Laurent-Désiré Kabila.

Etienne Kabila ameachiwa huru baada ya miaka miwili akiwa jela. Hata hivyo Mahakama kuu ya Pretoria haikutoa sababu za kuachiliwa kwa mwanasiasa huyo, lakini imesema kwamba huenda ikatoa maelezo zaidi Ijumaa hii.

Etienne kabila alikamatwa Afrika Kusini mwezi Februari mwaka 2013, ambapo alikua akiishi kwa miaka kadhaa.

Etienne Kabila alituhumiwa na watu wengine 19 kupanga njama za kuupindua utawala wa rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Joseph Kabila, hata hivyo vielelezo viliyotolewa na Mwendesha mashitaka vilikua hafitoshi, kwa mujibu wa majaji waliyosikiliza kesi hiyo.

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA