KIMENUKA! RAIS WA CHUO CHA CBE ABAMBWA NA MAMILIONI CHUMBANI



Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo cha Biashara (CBE), Ramadhan Kirungi.

Kwa mujibu wa chanzo makini, wizi huo unadaiwa kubainika baada ya makamu wake, Godfrey Modest kutumwa benki kwa ajili ya kutoa fedha ambazo cheki yake ilishasainiwa.“Yule makamu aliporudi chuoni alimweleza mhusika, akashagaa sana na hakuamini kilichotokea ndipo walipoamua kumkamata rais huyo.

“Walipokwenda kumkagua kwake walimkuta na shilingi milioni 16.5 keshi zilizosalia zikiwa zimefungwa katika mafungu matatu,” kilisema chanzo chetu kikiomba hifadhi ya jina lake.


Mamilioni aliyokutwa nayo.

Baada ya habari hizo kutua kwenye Gazeti la Amani, mapaparazi wetu walimtafuta msemaji wa chuo hicho, Leonidas Tibanga ambaye alikiri kutokea kwa wizi huo na kuongeza kuwa hatua zimechukuliwa na mtuhumiwa alikamatwa na kupelekwa polisi huku uchunguzi zaidi ukifanyika.“Ni kweli wizo huo umetokea na hivi ninavyozungumza na wewe, mtuhumiwa yupo polisi lakini uchunguzi zaidi unaendelea,” alisema Tibanga.

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA