MWANAFUNZI AFIA DARASANI KWA KUPIGWA NA MWENZIYE


Mwanafunzi wa darasa la tano katika shule ya msingi Ilola iliyopo katika wilaya ya Shinyanga vijijini aitwaye Veronica Venance mwenye umri wa miaka 12 amefariki dunia kwa kupigwa na mwanafunzi mwenzake wakati wakigombania daftari darasani kwa ajili ya kuandika notes.

Walioshuhudia tukio hilo wamesema limetokea Februari 24 mwaka huu, saa 7 na nusu mchana katika darasa la tano katika Shule ya Msingi Ilola iliyopo katika Kata ya Ilola, Tarafa ya Itwangi, Wilaya ya Shinyanga.

Wamesema mwanafunzi huyo amefariki dunia baada ya kupigwa makofi na ngumi sehemu za kichwani na mwanafunzi mwenzake aitwaye Sophia Mathew (12).

Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga limethibitisha kutokea kwa tukio hilo.

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA