CHADEMA YAWAPIGA 'STOP' WANAOTAKA KUWANG'OA LEMA NA NASSAR

1_697e8.jpg
Arusha. Chama cha Demokrasia na Maendeleo(chadema), mkoa wa Arusha "kimewapiga stop" wanachama wake, kutangaza nia ya kugombea ubunge katika majimbo matatu, yanayoshikiliwa na wabunge wa chama hicho,hadi hapo Bunge litakapovunjwa rasmi julai 2 mwaka huu.
Majimbo hayo ni jimbo la Arusha mjini, mbunge wake, Godbless Lema, Jimbo la Arumeru Mashariki, mbunge Joshua Nassari na Jimbo la Karatu mbunge, Mchungaji Israel Natse ambapo tayari kuna wanachama wa chama hicho, wameanza kutangaza nia za kuwang'oa wabunge hao.
Akizungumza na mwananchi leo, Katibu wa Chadema mkoa wa Arusha, Calist Lazaro alisema, maagizo anayoyatoa ni kutekeleza utaratibu ambao umetolewa na Kamati Kuu ya chama hicho,kuhusiana na uchaguzi mkuu ujao.
"Naomba hapa ieleweke kuwa hatuzuwii mtu kugombea lakini tunataka afuate taratibu ili kuzuia vurugu na kama mtu akikiuka sasa ina maana atakuwa amepoteza sifa"alisema Lazaro.
Lazaro alisema nia ya agizo hilo ni kuondoa vurugu na mpasuko ndani ya chama kabla ya wakati muafaka wa kutangaza nia na kuanza kampeni haujafika, lakini kwa majimbo yaliyo na wabunge wa CCM, wagombea wanaruhusiwa kutangaza nia.
Alisema chama hicho, kitatoa ratiba ya uchaguzi karibuni na fomu za kugombea nafasi mbali mbali zitapatikana katika ofisi za chama hicho, katika ngazi zote ila kwa maeneo yenye wabunge na madiwani wa chadema, fomu zitapokelewa bila kutangaza nia na kuanza kampeni.
Tamko hilo limekuja kukiwa na mpasuko mkubwa ndani ya Chadema katika majimbo hayo matatu, kutokana na idadi kubwa ya makada wa chama hicho, kuanza kunyemelea majimbo hayo. CHANZO: MWANANCHI

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA