AIBU! TICHA MBARONI KWA KUMUUZISHA MTOTO MAYAI MUDA WA SHULE

Deogratius Mongela na Chande Abdallah
MATUKIO ya mateso, unyanyasaji na utumwa kwa watoto yanashika kasi nchini! Safari hii mwalimu wa shule moja ya msingi iliyopo Mburahati jijini Dar aliyetajwa kwa jina moja la Lucy ametia aibu baada ya kutiwa mbaroni katika Kituo cha Polisi cha Magomeni, Dar akituhumiwa kumtumikisha mtoto mwenye umri wa miaka 12 aitwaye Sakina kwa kumuuzisha mayai ya kuchemsha na soseji.
Mwalimu huyo akijitetea juu ya sakata hilo.
Kwa mujibu wa mashuhuda wetu, tukio hilo lilichukua nafasi maeneo ya Kashuda Bar, Magomeni hivi karibuni baada ya wakazi wa eneo hilo kuhamaki kumuona binti huyo akitembeza mayai na soseji mtaani wakati umri wake ni mdogo kinyume na sheria za ajira.
RAIA WAMZUNGUKA
Ilisemekana kwamba, baada ya kukerwa na kitendo hicho huku Sakina akionekana hana furaha, raia hao wenye hasira kali walimhoji ambapo alimtaja mwalimu huyo kuwa ndiye bosi wake aliyemchukua kutoka Tanga kwa ajili ya kufanya kazi za ndani (hausigeli).
AFUATWA SHULENI
Ilidaiwa kwamba, wakifuatana na mtoto huyo, wakazi hao walifunga safari hadi shuleni kwa mwalimu huyo Mburahati ambapo wanahabari wetu walitonywa na kutia timu hadi kwa mkuu wa shule hiyo, Kibassa ambaye alikiri kuchukizwa na kitendo cha mfanyakazi wake kumwajiri mtoto wa miaka 12 kumtumikisha kazi akiwa ni mwajiri wa serikali.
Mwananfunzi Sakina anayedaiwa kuuzishwa mayai muda wa shule.
“Kimsingi nimesikitishwa kwa sababu Lucy ni mwajiriwa wa serikali, hapaswi kufanya jambo baya kama hili. Kwa umri wake alipaswa awe darasani,” alisema Kibassa.
MWALIMU AJITETEA
Kwa upande wake, Lucy alijitetea kuwa binti huyo aliletewa na mtu aliyemtaja kwa jina la Kizito aliyemuagiza mfanyakazi wa ndani, lakini baada ya kufika binti huyo alimkataa na kudai bado mdogo asingeweza kufanya kazi za ndani.
Mwalimu huyo alisema alikuwa akimsubiri binti mwingine mkubwa aletewe na Kizito ili amrudishe Sakina kwao na kudai kuwa hata biashara ya mayai hakumtuma yeye bali alimtuma John (kijana wake wa kazi) ila inawezekana Sakina alijiingiza kujisaidia na ugumu wa maisha.
Mwalimu huyo akiwekwa kikao.
BINTI ASIMULIA
Akiwa shuleni hapo, mbele ya bosi wake, Sakina alifunguka kuwa amekuwa akifanya biashara hiyo na kufanya kazi za ndani kwa Lucy huku akisimulia kunusurika kubakwa na kupitia mateso mengine kama kunyimwa chakula na kulazimika kutembeza mayai na soseji mchana kutwa.
“Nafanya kazi za ndani na kutembeza mayai, kuna kaka mmoja nilimwomba msaada ili nirudi nyumbani, akanilazimisha tufanye mapenzi ndipo anisaidie, nilipokataa akaniacha,” alisema Sakina.
Hata hivyo, mwalimu huyo alitolewa shuleni hapo chini ya ulinzi mkali kisha kufikishwa Polisi Magomeni katika dawati la jinsia kwa hatua zaidi.
UNGANANASIKATIKAFACEBOOK,TWITTER,INSTAGRAM,YOUTUBE    

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA