NDOA YA SLIM YAVUNJWA MAHAKAMANI



“Mahakama hii imevunja baada ya mdai (mke) kusema hata iweje hawezi kurudi tena kwa mumewe huyo kutokana na kuwa na wivu wa kupindukia na kingine kibaya walivyokuwa kwenye mgogoro kuna mwanamke alikuwa akijinadi  kwa kupiga picha nyumbani kwa mumewe na kuzituma kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram,” alisema Hakimu Mwanaidi Madeni wa mahakama hiyo.

Hakimu aliamuru watalaka hao kugawana mali zote walizochuma pamoja likiwemo gari walilozawadiwa wakati wa harusi yao, ambalo ndilo lilikuwa chanzo cha mgogoro huo.Wakati mume akisema anaiheshimu hukumu hiyo ingawa anaona kama ni filamu, mke alionyesha furaha yake na kudai sasa ataishi kwa amani.

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA