MSANII WA FILAMU ZA KIBONGO, DOREEN REGUNA ‘QUEEN MAGAL AIBUKA NA MIMBA YA MEZ B



Msanii wa filamu za Kibongo, Doreen Reguna ‘Queen Magali’.

Akizungumza  huku akionesha sura ya masikitiko, Queen Magali alisema kinachomuuma zaidi ni kwamba, ujauzito wa marehemu aliokuwa nao, ulichoropoka saa chache baada ya kupokea taarifa za msiba huo.

“Nilipopigiwa simu kwa mara ya kwanza, sikuamini, hata ndugu zake marehemu walinipigia simu, sikuamini hadi nilipompigia shangazi yake ambaye alinithibitishia msiba huo, hapohapo nikapata mshutuko, hali yangu ikawa mbaya hadi nikalazwa.

“Nashukuru Mungu kwa sasa naendelea vizuri.
“Kiukweli msiba huu kwangu umekuwa ni pigo kubwa, tulikuwa na mipango mingi na marehemu katika maisha yetu, alishanitambulisha kwa ndugu na jamaa zake wote wa karibu lakini nasikitika zaidi kwa kuwa nimechelewa kuhudhuria mazishi ya mpenzi wangu kutokana na kuzidiwa ghafla lakini nitafanya kila liwezekanalo ili nikaweke japo mchanga kwenye kaburi la mtu niliyempenda katika maisha yangu,” alisema Queen Magali.

Baadhi ya wapenda ‘ubuyu’ waliokuwa wakisikiliza mahojiano ya Queen Magali na mwanahabari wetu, walisikika wakihoji kwa nini mrembo huyo asianike uhusiano wake na Mez B kabla hajafariki lakini mwenyewe alidai walikubaliana uchumba wao uwe wa siri.
Mez B alifariki dunia nyumbani kwao Dodoma Ijumaa iliyopita ambapo alizikwa katika makaburi ya Wahanga wa Reli, Dodoma.

chanzo:GPL

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA