shindi wa milioni 100/= kwa siku akosekana! Wateja wa Vodacom changamkieni promosheni ya JayMillions
- Mshindi wa milioni 100 kwa siku, washindi wa milioni 10 na washindi wa milioni 1/-wakosekana
- Wateja wahimizwa kutuma neno Jay kwenda 15544 kila siku kujua kama wameshinda
Dar es Salaam, Tanzania, Januari 15, 2015: Wateja wa kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania wametakiwa kuchangamkia promosheni ya Jaymillions ambayo ilizinduliwa juzi ili waweze kujishindia mamilioni ya fedha kwa kuwa droo ya kwanza iliyofanyika leo/jana mshindi wa milioni 100/- hakupatikana wakiwemo washindi kumi wa milioni 10/- na washindi mia moja wa shilingi milioni 1/-.
Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Kelvin Twissa alisema leo baada ya kumalizika droo ya kwanza:“Natoa wito kwa wateja wetu kuangalia namba zao kama zimeshinda kila siku kwa kutuma neno JAY kwenda namba 15544 ili kutopoteza nafasi za ushindi kwa siku. Vodacom itatoa mshindi mmoja wa Sh.100m/- kila siku, washindi kumi wa Sh.10m/- kila siku na washindi miamoja wa Sh.1m/- KILA SIKU kwa siku mia moja! Pia washindi elfu kumi watapokea muda wa maongezi wa bure wenye thamani ya Sh. 1000/- hivyo nawasihi wateja wetu kuchangamkia hii fursa muhimu”.Alisema.
Twissa aliongeza kusema kuwa mara tu ujumbe huu unapotumwa, mteja atapokea ujumbe mfupi utakaomjulisha kama ameshinda na ikiwa hajashinda siku hiyo atajulishwa hivyo na kuambiwa ajaribu tena siku inayofuata. Kila SMS itagharimu Sh. 300/- tu.
Alisisitiza kuwa kila siku namba zilizoshinda zitapatikana kupitia mfumo mahsusi wa promosheni hii na aliwahimiza wateja kuhakikisha wameangalia kila siku kama namba zao zimeshinda ili wasipoteze bahati zao iwapo namba zao zitakuwa zimechaguliwa. Bila kufanya hivyo, wanaweza kupoteza mamilioni kama ilivyotokea leo katika droo ya kwanza kwani hawatoweza kujua kama namba zao zilichaguliwa kama washindi ambapo zinachaguliwa kila siku.
Alimalizia kwa kusema kuwa promosheni hii inathibitisha dhamira ya kampuni ambayo mbali na kutoa huduma bora kwa wateja wake pia ina dhamira ya kubadilisha maisha ya wateja kuwa murua zaidi ambao wamekuwa wakiendelea kujiunga na familia ya Vodacom na kuwataka kushiriki kwa wingi.
Katika droo ya leo washindi wapatao 116 wameweza kujishindia muda wa maongezi.

Comments
Post a Comment