Posts
Showing posts from September, 2014
NAFASI ZA KAZI KOPLO NA KONSTEBO WA UHAMIAJI ZIMETANGAZWA TENA, SOMA HAPA
- Get link
- X
- Other Apps
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi anatangaza nafasi za kazi zifuatazo katika Idara ya Uhamiaji kwa Raia wote wa Tanzania wenye sifa. 1. KOPLO WA UHAMIAJI Nafasi 114 - (Nafasi 100 kwa ajili ya Tanzania Bara na Zanzibar na nafasi 14 maalum kwa ajili ya Zanzibar tu) A. SIFA ZA MWOMBAJI: (i) Awe Raia wa Tanzania mwenye umri kuanzia miaka 25 hadi 30. (ii) Awe amehitimu kidato cha sita na kufaulu masomo ya Kiingereza, Kiswahili, Historia, Jiografia, Kifaransa, Hisabati ambapo masomo mawili kati ya hayo yawe katika kiwango cha “Principal”. (iii) Awe pia na mojawapo ya sifa zifuatazo: Cheti cha Sheria; Cheti cha Kompyuta; Cheti cha Ufundi (FTC) kwenye fani ya umeme na mitambo (iv) Waombaji wenye ujuzi wa mojawapo ya lugha zifuatazo (Kifaransa, Kichina, Kijerumani, Kiarabu au Kihispania) watafikiriwa kwanza. (v) Aidha, Mwombaji a...
WANACHUO 58 WAPOTEA MEXICO
- Get link
- X
- Other Apps
Mama wa mmoja wa wanachuo walotoweka Polisi wa kusini mwa Mexico katika mji wa Guerrero wanawasaka wanachuo 58 wa chuo cha ualimu ambao hawajulikani waliko tangu yalipotokea mapigano baina ya polisi na wanachuo hao mwishoni mwa wiki . Wanafunzi hao ni kutoka katika chuo cha ualimu inasemekana walitoweka baada ya kukabiliana na polisi wakati wa maandamano. Katika makabiliano hayo na askari watu sita walipoteza maisha na wengine kumi na saba walijeruhiwa wakati mtu mwenye silaha alipowashambulia waandamanaji hao na abiria waliokuwa kwenye basi katika kijiji cha Iguala. Wanachuo hao wa chuo cha ualimu waliinggia kwenye maandamano kupinga upendeleo wa wanachuo wenzao wa mjini kupendelewa zaidi katika nafasi za mafunzo kazini kuliko wa kutoka vijijini. chanzo:BBC
PICHA: HONG KONG BADO HALI TETE
- Get link
- X
- Other Apps
Raia wa Hong Kong wakivurumushiwa moshi Makumi kwa mamia ya waandamanaji wa Hong Kong wanaendelea na maandamano yao kwa siku nyingine tena baada ya kudhoofisha maeneo muhimu ya jiji hilo wakati wa mchana. Waandamanaji hao sasa wanamtaka Mkuu wa utawala wa Hong Kong Leung Chun-Ying ajiuzulu.. Wakati huo huo Marekani imesema inafuatilia kwa karibu kinachoendelea Hong Kong na imeutaka utawala kuchukua hatua. Katika mkutano wa wanahabari msemaji wa Ikulu ya Marekani Josh Earnest amesema Marekani inaunga mkono matakwa ya watu wa Hong Kong. "Duniani kote, na hii ni kweli katika Hong Kong na maeneo mengine, Marekani inaunga mkono kimataifa, uhuru, kama vile uhuru wa kukutana kwa amani na uhuru wa kujieleza. Marekani inautaka utawala wa Hong Kong kuchukua hatua, na kwa upande wa waandamanaji kutoa maoni yao kwa amani" chanzo:bbc
PAKA AFUNGIWA HIRIZI MTINI
- Get link
- X
- Other Apps
Tukio hilo lililokusanya umati mkubwa wakiwemo waumini wa msikiti huo lilitokea alfajiri ya Alhamisi iliyopita ambapo… Stori: Dustan Shekidele, MOROGORO KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida, paka mwenye hirizi kubwa shingoni akiwa hai alikutwa amepigiliwa misumari juu ya mti uliopo jirani na Msikiti wa kwa Mtawara uliopo Kata ya Mwembesongo mkoani hapa. Paka mwenye hirizi kubwa shingoni akiwa amepigiliwa misumari juu ya mti uliopo jirani na Msikiti wa kwa Mtawara uliopo Kata ya Mwembesongo, Morogoro. Tukio hilo lililokusanya umati mkubwa wakiwemo waumini wa msikiti huo lilitokea alfajiri ya Alhamisi iliyopita ambapo baadhi ya waumini wa msikiti huo walikuwa wamefika msikitini kwa Swala ya Alfajiri. Baadhi ya waumini wa msikiti huo walipohojiwa na mwandishi wetu walisema alfajiri hiyo walisikia sauti ya paka akilia kutoka kwenye mti huo uliopo kandokando ya Barabara ya Mtawara inayoelekea Kichangani na Mji Mpya. Watoto wakishudia tukio hilo la kushangaza. “Tulifika...
Chahali: Maoni yangu - JK aziponda sera za uchumi za Nyerere, adai zimechangia umasikini wa Tanzania
- Get link
- X
- Other Apps
. Rais Jakaya Kikwete amezilaumu sera za uchumi za Tanzania baada ya nchi yetu kupata uhuru akidai zimepelekea hali duni ya kiuchumi. Alieleza kuwa sera hizo ni moja ya sababu zinazoifanya Tanzania kuwa katika kundi la Nchi Masikini Zaidi Duniani (The Least Developed Countries - LCD) tangu utaratibu huo wa kuzigawanya nchi kutokana na viwango vyake vya kiuchumi na maendeleo uanze miaka ya 70. Akihutubia Alhamisi iliyopita jijini Washington DC, nchini Marekani katika Kongamano la Shirika la Misaada la nchi hiyo (USAid Forum) kuhusu vikwazo vya maendeleo na jinsi ya kutokomeza umasikini uliokithiri, Rasi Kikwete alisema kwamba itikadi iliyoongozwa na kuaminiwa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere imeshindwa kuzaa matunda. Akieleza kwanini nchi 33 kati ya 48 masikini zaidi duniani zipo Afrika, Rais alieleza kuwa nyingi ya nchi hizo (25) ni wahanga wa migogoro, lakini baadhi kama Tanzania zimekuwa na amani na utulivu lakini zimeendelea kuwa katika kundi hi...
BOB HAISA -"LAMSONDO" (OFFICIAL MUSIC VIDEO) DIRECTED BY KENNY UKIYZ
- Get link
- X
- Other Apps
ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA VYUO VYA UALIMU 2014/2015 NGAZI YA CERTIFICATE NA DIPLOMA
- Get link
- X
- Other Apps
WALIOCHAGULIWA VYUO VYA UALIMU 2014/2015 WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI WAOMBAJI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA UALIMU NGAZI YA STASHAHADA YA JUU (MIAKA 3) MWAKA WA MASOMO 2014/2015 MAELEKEZO: Waombaji waliochaguliwa kujiunga na Mafunzo ya Ualimu mwaka wa masomo 2014/2015 wanatakiwa kuripoti katika Vyuo walivyopangiwa tarehe 06/10/2014 . Fomu za maelekezo (Joining Instructions) zitatolewa na chuo husika na zitatumwa kwa waliochaguliwa tu. Waliochaguliwa wanatakiwa kufika vyuoni wakiwa na mahitaji yaliyoainishwa kwenye fomu ya kujiunga na Chuo. Aidha, fomu hizi zinapatikana pia kwenye Tovuti ya Wizara:www.moe.go.tz; NACTE:www.nacte.go.tz; na TAMISEMI: www.pmoralg.go.tz Muhimu: 1. Waombaji waliochaguliwa ni wale wenye ufaulu wa Daraja la I hadi III 2. Waliochaguliwa wanatakiwa kuwasilisha Vyeti halisi vya Baraza la Mitihani la Tanzania Kidato cha NNE na SITA (CSEE na ACSEE) na vyeti vya kuhitimu Elimu ya Sekondari na M...