PICHA: WAFANYABIASHARA WA MANISPAA YA MUSOMA WAGOMA KUFUNGUA MADUKA
Wafanyabiashara wa Manispaa ya Musoma wameingia katika mgomo wa kutokufungua maduka kwa kupinga mashine za kielectroniki za EFD, mgomo huu umekuwa sio wa kwanza kutokea mkoani Mara na sehemu nyingine hapa nchini katika kugomea matumizi ya mashine hizi katika kukusanyia mapato ya serikali.
Serikali kupitia mamlaka ya ukusanyaji kodi (TRA) iliamua kuanzisha mashine hizi za kielectroniki ili kudhibiti ukusanyaji wa kodi,lakini mashine hizi zimeendelea kuwa mwiba kwa wafanyabiashara kwa kulalamika ghrama kubwa za kununua mashine lakini pia kodi kubwa inayokatwa katika kila bidhaa ambapo bidhaa inaweza kukatwa kodi si chini ya mara 3 mpaka kumfikia mtumiaji wa mwisho.
Comments
Post a Comment