WATU SITA WAHUKUMIWA KWENDA JELA NA KUCHAPWA MIJELEDI 91 BAADA YA KUCHEZA WIMBO WA PHARRELL WILLIAM "HAPPY" KWENYE KANDA YA VIDEO.
Watu sita nchini Iran waliokamatwa baada ya
kuonekana kwenye kanda ya video iliyokuwa inaiga wimbo wa 'Happy' wake
mwanamuziki mashuhuri Pharrell William, wamehukumiwa kifongo cha hadi
mwaka mmoja jela kila mmoja pamoja na adhabu ya kuchapwa mijeledi 91.
Wakili
wa sita hao amesema kuwa hukumu hiyo itaahirishwa kwa miezi sita
ikmaanisha kuwa watafungwa tu jela ikiwa watarejelea kosa hilo.
Kanda
hiyo inaonyesha wanaume watatu na wanawake watatu ambao hawajafunika
vichwa vyao wakicheza densi kwenye barabara na katika paa za nyumba
mjiniTehran.
Kanda hiyo iliyowekwa kwenye mtandao wa kijamii wa You Tube, imetazamwa na zaidi ya watu milioni moja.
Wengi
wa waliohusika kuitengeza kanda hiyo, walifungwa kwa miezi sita , huku
mmoja wao akifungwa kwa mwaka mmoja, alinukuliwa akisema wakili wao
Farshid Rofugaran.
Kanda hiyo kwa jina, "Happy we
are from Tehran" ilifikishwa kwa maafisa wakuu nchini Iran mwezi Mei
baada ya kutazamwa na watu 150,000 kwenye You Tube.
Waliohusika
pia walikamatwa na kushitakiwa kwa kosa la kukiuka sheria za kiisilamu
ambazo zinawazuia wanaume kucheza densi na wanawake na pia wanawake
kutoka nje bila hijab.
Baadaye washukiwa walionekana kwenye televisheni wakijitetea kwamba wao ni waigizaji walihadaiwa kushiriki katika kanda hiyo
Kukamatwa
kwa vijana hao kulizia ghadhabu kutoka anga za kimataifa huku watetezi
wa haki za binadamu wakianzisha kampeinii kwenye mitandao ya kijamii
kutaka waachiliwe.
Mwanamuziki Paharrel Williams mwenyewe, ambaye
wimbo wake huo, uliteuliwa kwa tuzo la Oscar, pia alieleza kukerwa na
kukamatwa kwa watu hao.
"inachukiza kwamba vijana waliokuwa tu wakijaribu kujifurahisha wanakamatwa,'' aliandika kwenye ukurasa wake wa Facebook.
Chanzo:bbc swahili.
Comments
Post a Comment